Abrahamani Kinana, Katibu mkuu wa CCM |
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abrahaman Kinana amesema wananchi hawapashwi kuwalalamikia viongizi wao wa chini na lawama zao kuzitupia kwa viongozi wa juu.
Alisema mambo yote yaliyoahidiwa utekelezaji wake unatoka katika uongozi wa juu hivyo wananchi wasiwachukie viongozi wa ngazi za chini kwani wao ni kama wananchi wa kawaida na maisha yao ni ya kawaida.
"Viongozi hawa wa ngazi ya chini hampashwi kuwachukia kwani hawa ni viongozi wa kawaida ambao mnaishi nao maisha ya kawaida lakini lawama hizo ya kutotekelezewa hahadi zenu zitupieni kwa uongozi wa juu kwani nio wanao paswa kulaumiwa kwa kutotekeleza ahadi," Alisema Kinana
Kinana alisema, anailaumu CCM kwa kutotimiza ahadi zake ambazo iliziahidi wakati wa kampeni hivyo kuwafanya wananchi kukichukia chama hicho.
Alisema, wananchi wanaweza kuto kirudisha chama hicho madarakani kutokana na kutoona manufaa ya chama hichu kutoka na kuto timiza ahadi zilizo tolewa wakati wa kampeni.
Alisema, wapinzani wataichukua Nchi kutoka na uongo uliopo ndani ya Chama hiki kwa kutotekeleza haadi ambazo ziliwafanya wananchi kutuchagua.
Aliongeza, kwa kutoa mfano kuwa katika Nchi ya jirani ya Zambia kuna viongozi wengi walikuwa wakitolewa madarakani kutoka na kuto timiza ahadi za ilani zao walizo kuwa wakizitoa wakati wa uchaguzi.
Alisema, katika nchi hiyo mpata wananchi wakaamua kuchagua chama pinzani ili waone utofauti wa chama kilichotawala kwa mda mrefu lakini wamekutana na yaleyale ya kuto timiziwa ahadi zao kwa kuambiwa waendelee kusubili.
Aidha, kwa kufanya hicho CCM ina wapoa ushindi wa bure wapinzani kwani wanayajua mazaifu ya chama hicho na kuwaambia wananchi mazaifu hayo.
Hivyo Kinana alisema, mbali na mapungufu hayo ambayo yapo wazi kutoka katika chama Hicho alisema kuwa chama hicho kimefanya mambo mengi ambayo wananchi wanapashwa kukishukuru.