Brotherhood wachoma moto vyuo vikuu



Kundi la Muslim Brotherhood kilichopigwa marufuku nchini Misri wamechoma moto majengo ya vyuo vikuu viwili katika mji mkuu wa Cairo.
Wanafunzi walikuwa wakiwapiga polisi katika eneo la Chuo Kikuu cha al-Azhar , mjini Cairo.
Watu watatu waanarifiwa kufa siku ya ijumaa wakati polisi walipokuwa wakipambana na wafuasi wa Muslim Brotherhood katika eneo la Minya ya Kusini na Nile Delta.
Mamlaka nchini Misri imekuwa ikiwasaka kundi la Muslim Brotherhood tangu mwezi julai, wakati aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi ambaye ni mfuasi wa kundi hilo alipoondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo.
Tayari kundi hilo limeshatangazwa kuwa ni kundi la kigaidi tangu jumatano.
Na BBCswahili