YAFAHAMIKA - MESSI ANGEWEZA KUSAJILIWA NA CHELSEA KAMA MOURINHO ANGELIPA £105m


Lionel Messi angeweza kujiunga na Chelsea katika dirisha la usajili lilopita baada ya kampuni ya vifaa vya michezo adidas kutoa of a ya kulipa nusu ya fedha zake za usajili 
£210million, hii ni kwa mujibu wa gazeti la michezo la Barcelona Mundo Deportivo.
Messi, ambaye alijiunga na Barcelona akiwa na miaka 13 na klabu hiyo ilimlipia ada ya matibabu ya ugonjwa wake wa upungufu wa homoni za ukuaji, sikh zone amekuwa na mahusiano mazuri na klabu hiyo. 
Lakini kwa mujibu wa Mundo Deportivo, adidas waliona nafasi/fursa ya kumchukua nyota huyo kutoka Barca na pia kwa wadhamini wa klabu hiyo ya Catalan - Nike - na kumpeleka kwenye moja ya timu wanazozidhamini barani ulaya: Chelsea, Bayern Munich au Real Madrid.
   

Mundo linasema kwamba wawikilishi wa Messi walikuwa wameshafahamishwa lento hilo la adidas na kwamba na wao walishafahamisha klabu - ambao waliwajibu kwamba hawakuwa tayari kumuuza Messi.

Hata kama adidas wangelipa hiyo £105m, Chelsea bado wangetakiwa kulipa kiasi cha  £105m na mocha Jose Mourinho ingebido afanye kazi kubwa kumshawishi mchezaji ambaye hakuwahi kuwa na mahusiano nae mazuri. 

Raisi wa Real Madrid Florentino Perez angetakiwa kulipa fdha nyingi kuliko alizolipa kumnunua Luis Figo mwaka 2000 kama angetaka kumsaini Messi. 
Habari hizi za Michezo na  Shaffih Dauda