WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA KUKAMILISHA MAPEMA UJENZI W MFEREJI



KATAPILA KIKIENDELEA NA KAZI YA UCHIMBAJI WA MFEREJI WA MAJI



WANANCHI wa vijiji saba vya halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya vinavyo tarajia kutumia mradi wa umwagiliaji wa Mwendamtitu ulioibuliwa na wananchi hao kuwasaidia kuukamilisha kwa wakati.


Wakizungunza kwa nyakati tofauti katika mradi huo wananchi hao wamesema kuwa selikali iliwachangia kujenga katika sehemu ya banio kutoka katika mto mkubwa katika mradi huo.

Katibu wa wakulima katika mradi huo wa Mwendamtitu wilayani humo, Peter Mwitanye alisema kuwa wananchi wa vijiji saba vitakavyo nufaika na mradi huo wamechanga fedha kwaajili ya kuchimba mfereji ambao utatoa maji kutoka katika banio hadi mashambani.

Mwitanye alisema kuwa serikali ya halmashauri ya Mbarali iliwaperekea katapila ambaro waliambiwa watachangia mafuta lakini limekuwa likitumia fedha za mafuta katika matengenezo na kazi kusimama kwa mda mrefu.

Wananchi baada ya kuona hivyo waliamua kukodi makatapila mawili ili kuhalakisha ujenzi wa mifeleji hiyo ili kukamilisha mradi huo kumamilika kwa mapema.

“Wananchi kutoka katika vijiji saba wanaotarajia kuutumia mfereji huu wamechangafedha ambazo tumetumia kukodi makatapila mawili ambayo yanachima mfereji huu yakiwa yamegawanyia moja likiwa limeanzia mwanzo na linguine lipo mwishoni mwa mradi,” alisema Mwitanye.

Alivitaja vijiji vitakavyo nufaika na mradi huo kuwa ni pamoja na Mwakaganga, Tyego, Lunda, Imalilosongwe, Mila, Mwanavala, Nyelegete na taasisi mbili ambazo ni shule ya Mount Fort na St. Ana zilizopo wilayani humo karibu na mradi huo.

Baadhi ya wananchi waliliambia Elimtaa kuwa wamekuwa wakichanga michango hiyo ili mradi huo uende kwa haraka na kukamilika kwa wakati kabla ya msimu wa kilimo ambao umekaribia.

Waliiomba serikali kuchangia mradi huo ili kukamilika kwa mradi wao huo ambao ukikamilika watabaikiwa na changamoto ya kibali cha kuyatumia maji kutoka kwa mamraka ya bode la Rufiji.

Fred Kangw’ata mkazi wa maeneo ya mradi huo alisema kuwa serikali iwasaidie kuukamilisha mradi kuo kwa wakati kwani itawakomboa katika kaisha yao na kuwaondoa katika masuala ya umaskini.