WATABIBU wa tiba za asili mkoani Mbeya wamelaani vikali
kitendo cha baadhi ya watabibu na waganga kujihusisha na ushirikina na hasa
tukio lililotokea jijini Mwanza kwa
wanga wa kienyeji kufanya vitendo vya ajabu na kutaka visijirudie.
Hayo yamebainishwa na watabibu wa tiba za asili Juzi wakati
wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kutoa tamko la kulaani vitendo vya
ajabu vinavyofanywa na waganga wa jadi na kusababisha uvunjifu wa amani.
Mratibu wa taasisi ya watabibu wa tiba za asili Tanzania
(ATME) mkoa wa Mbeya, Boniventure Mwalongo, alisema kuwa wanalaani vikali vitendo vya kikatili vinavyofanywa
na waganga wa tiba za asili.
“Nashukuru viongozi wa vyama vya watoatiba za asili mkoa wa
Mbeya, kwa ushirikiano wenu na kukutana kwa pamoja kulaani vitendo vibaya
vilivyo fanywa na waganga wa jadi wawili jijini
Mwanza vya kikatili na hatimaye kukutwa na mikino ya
binadamu,” Alisema Mwalongo
Alisema kuwa vitendo hivyo havikubaliki na wanapinga vikali
na hawataki vikatokea mkoani Mbeya kwani ni aibu kwa taaluma yao ya utabibu.
Kwa upande wa washiliki ambao ni viongozi wa watabibu mkoa wa
Mbeya wamesema kuwa vitendo hivyo havi fai kutokea na watabibu na wakunga wa
jadi wanalaani na wanaomba sheria kali zichukuliwe kwa wale watakao kamatwa
wakijihusisha na ukalili wa aina hiyo.
Mmoja wa watabibu hao, Addala Azizi alisema kuwa wao kama
watoa tiba za asili wa mkoa wa Mbeya wanalaani vitendo vya aina hiyo
visijirudie mahali popote Tanzania na hawapendi vitokee.
Nae Zahara Masudi alisema kuwa tatizo limekuwa ni kwa wateja
na sio kwa waganda wa jadi kwani ndio wanao washawili kufanya vitendo hivyo.
Alisema kuwa binadamu tunazalilika kwa kufikili mambo ya
ajabu na tunayo yafanya hasa wale wanao kuwa na ufinyu wa kufikili na kuwaza
kuwa wanaweza kupata utajili ama kupona baada ya kumuua mtu mwingine huo ni
upungufu wa akili.
Serikali itunge sheria kali kwaajili ya kuwabana watakao
kamatwa wakijihusisha na mambo ya ajabu na kufanya matukio ya kishirikina.
Watabibu hao walikutana baada ya kutokea tukio la ajabu
lililotokea mkoani mwanza mwishoni mwa mwezi uliopita la mganga wa jadi kudaiwa
kukutwa na kiganja cha mkono wa binadamu.