CWT MBEYA YASIKITISHWA NA KAULI YA SERIKALI KUHUSIANA NA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE



CHAMA cha waalimu Mbeya kimesema hakijalizika na kimeumia kufuatia uamuzi wa Serikali wa kushusha madaraja katika mtihani wa kidato cha nne.

Akizungunza na waalimu wa Mkoa wa Mbeya katika uzinduzi wa jingo la chama chao mkoani Mbeya, Mwenyekiti wa Chama waalimu Tanzania CWT Mbeya, Nelusingwe Kajuni, alisema kuwa anashangaza na ameumia sana kufuatia kitendo cha kushusha madalaja ya ufaulu wa wananfunzi kidato cha nne.

 Alisema kuwa Serikali badala ya kuongeza kasi ya kuongeza vitendea kazi na kuongeza kasi ya kufundisha wanafunzi na wakafauru kwa wingi wanashusha madaraja.

Alisema kuwa hatua hiyo imewaumiza sana waalimu na hawajapendezewa na mfumo inao kwendanao kwani wanaenda kuishusha elimu ya Tanzania na kuwa na vijana wasio na uwezo wengi zaidi.

 Kajuni alisema kuwa kwa kufanya hivyo tutapata sifa nje ya nchi kufuatia kuonekana wanafunzi wengi wamefaulu na kuwa na idadi kubwa ya vijana walio faulu huku walio pata wastani wa chini niwengi kuliko walio fauru.

Nae Rais wa CWT taifa Gration Mukoba alisema kuwa serikali imekuwa na mkanganyiko kufuatia suala hili la kuongeza madalaja ya ufauru.

Alisema kuwa serikali imekuwa na kauli tofauti kufuatia madalaja hayo ambapo Waziri wa Elimu, Dkt. Shukuru Kawambwa , anasema kauli ya Waziri ni kauli ya Serikali na alisema hakuna ziro huku Naibu Waziri wake Philipo Mulugo alisema kuwa ziro ipo ila madalaja yameongezeka.

Mukoba alisema kuwa baada ya kauli hizo mbili pia kuna kauli ambazo zinagongana tena akaibuka Spika wa Bunge Anna Makinda na kuwema kuwa inatakiwa itolewe kauli moja yenye msimamo kati ya hizo mbili zilizo tolewa na viongozi hao.