Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd.
Chedi Ngulu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya
maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Bodi ya ushauri wa Umoja wa
Afrika ya kupambana na Rushwa yaani African Union Advisory Board on
Corruption (AUABC) na Tamasha la wasanii lenye lengo la kufikisha
ujumbe juu ya Madhara ya Rushwa kwenye Jamii, Kati kati ni Emmanuel
Atenga toka (AUABC) na Stephane Ndilimbaye toka AUABC.
Na.Mwandishi wetu
TAASISI YA KUPAMBANA NA KUZUIA RUSHWA
(TAKUKURU) kwa kushirikiana na Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika katika
Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC) na Megamark Ltd wameandaa tamasha
kubwa litakalowashirikisha wasanii mbali mbali toka Tanzania, Kenya na
Uganda katika kuadhimisha miaka 10 tangu bodi hiyo ya Afrika katika
maswala ya Rushwa kuanzishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari
makao makuu ya Takukuru jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa
Megamark ltd, Chedi Ngulu amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni
kufikisha ujumbe kwa umma juu ya kupambana na Rushwa na kuelezea madhara
ya Rushwa kwenye jamii na nchi kwa ujumla.
Bw. Emmanuel Atenga (wa pili kushoto) kutoka na Bodi ya Ushauri wa Umoja wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Rushwa (AUABC)
akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tamasha hilo litakalofanyika
tarehe 7 mwezi ujao katika viwanja vya General Tyre Arusha. Kulia ni
mmoja wa wasanii wataoimba kwenye Tamasha hilo Fid Q na wa pili kulia ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Megamark Ltd. Chedi Ngulu na kushoto ni Stephane Ndilimbaye kutoka AUABC.
“Muziki upo katika asili ya waafrika
na umekuwa ukitumika kuburudisha lakini zaidi kufikisha ujumbe wenye
kujenga na kurekebisha jamii (Hadhira) iwe ni nyimbo, kughani ambayo
tunatambua kwa njia ya Rap na ngoma za asili, lakini tumechagua muziki
kama njia rahisi ya kufikisha ujumbe hasa kwa vijana kuhusu madhara ya
Rushwa,” amesema Ngulu.
Amesema kuwa katika tamasha hilo
nyimbo mbalimbali zitaimbwa katika kuelezea matatizo ya Rushwa kwenye
jamii na hasa kuelimisha vijana umuhimu wa kukataa Rushwa kwa sababu
vijana ndio nguvu kazi ya taifa na asilimia 75 ya watu nchini ni vijana.
“kwa mantiki hii, tumeandaa onyesho
lenye anuani isemayo “Rushwa sio” ikimaanisha rushwa haina manufaa na ni
yenye kutakiwa kupigwa vita kwa gharama yoyote ile,”
Msanii Fid Q akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo.
“Onyesho hili litafanyika Arusha
tarehe 7 mwezi wa kumi na mbili katika viwanja vya General Tyre kuanzia
saa saba na nusu mpaka saa kumi na mbili jioni na litahusisha wasanii
wenye kukubalika na jamii,” alisisitiza
Kwa upande wake, Emmanuel Atenga toka
Kitengo cha Mawasiliano (AUABC) amesema Board hiyo ya Umoja wa Afrika
ya kupambana na rushwa imepata mafanikio kwa kuanzisha vitengo vya
ufatiliaji kwa wanachama wa Umoja wa Afrika wenye lengo la kusaidiana
katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Amesema mapambano dhidi ya rushwa
Afrika yanahitaji nguvu ya pamoja kwa ksuhirikisha jamii wakiwemo
wasanii katika kuhamasisha mapambano ya kukataa Rushwa kwenye ngazi zote
ndani ya nchi na bara zima la Afrika.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe,Muhibu Said akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
habari na Mkonowangu Blog