WAKURUGENZI
wa halmashauri na watendaji serikalini wametakiwa kuwahimiza wananchi
wa kujiunga na mfuko wa jamii wa afya (NHIF) ili kujikinga na masuala ya
magonjwa na kufikia malengo ya kusajili kaya nyingi.
Hayo
yamebainishw ana mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandolo, alisema kuwa
wakurugenzi waweke mikutano ya kuhamasisha wananchi kujiunga na NHIF na
kuulizana kwanini wanachama hawaongezeki.
Amesema
kuwa wakurugenzi na watendaji katika halmashauri mkoani mbeya
wajitahidi kufika katika kila kona ya halmashauri ili kuhamasisha
wananchi kujiunga na mfuko huo.
Alisema kuwa kuwa halmashauli nzitenge fedha kwaajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kijiunga na taasisi hiyo ya kiafya.
Alisema halmashauri pia zichukue hatua ya kuhakikisha vituo vinavyo toa huduma kutoa huduma bora kwa wateja wanaohuduma.
Alisema kuwa wananchi wakijiunga na mifuko hii itawasaidia wananchi watakao ugua kupata hudiuma hiyo hata kama hana pesa.
Kwa
upande wake Kaimu mkurugenzi mwezeshaji wa NHIF Grece Lobulu alisema
kumekuwa na ongezeko la taratibu kwa wananchi wanao jiunga na mfuko huo.
Alisema
kuwa asilimia kumi na moja mkoani Mbeya wameongezeka na kwa mwaka ujao
wanahitaji kuwafikia wananchi wengi ili kufika mwaka 2015 kuwafikia
wananchi wengi hadi asilimia 35.
Amesema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali za baadhi ya wananchi kutumia kadi moja kwa wananchi zaidi ya mmoja na wanajitahidi kukabiliana na changamoto hiyo.