Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi wakamilika

Mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yamekamilika mjini Warsaw. Awali nchi mbili zinazotoa kiwango kikubwa cha gesi  zinazochafua  mazingira, China na India zilipambana vikali na Marekani pamoja nchi nyingine kuhusiana na ya kuyaandika mapendekezo yaliyokuwa yakijadiliwa. 
Lakini jana, wawakilishi kutoka takribani nchi 200 walikubaliana kuhusu maamuzi hayo. Makubaliano hayo yanaruhusu mkataba mpya kuhusu utoaji wa gesi ya kaboni kuidhinishwa mnamo mwaka wa 2015. 

Kongamano hilo pia liliujadili mpango wa kupunguza uharibifu wa misitu. 
Ujumbe wa Ujerumani katika mkutano huo ulisema maamuzi hayo yanaonyesha dalili kubwa kwamba hata baada ya kutokea tofauti katika mazungumzo hayo, bado wajumbe waliweza kulegeza misimamo yao na kufikia mapatano. 
Habari na DW.DE