WATU WANANO WAFA, NI KWA VIPIGO VYA MAWE, KUCHOMWA MOTO

  • Wachomwa moto baada ya kufumaniwa
  • Wapigwa mawe marungu baada ya kuuwa kwa tuhuma za ushirikina

WATU watono wamekufa katika matukio mawili tofauti likiwemo la watu wawili kuteketezwa kwa moto wakiwa ndani wamelala huko katika kijiji cha Magamba wilayani Chunya kwa kisa cha wivu wa kimapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Robert Mayala alisema kuwa katika tukio la kwanza juzi majira ya saa 3:00 usiku, watu wawili waliteketea kwa moto wakiwa ndani wamelala usiku.

Aliwataja marehemu hao walioteketea kwa moto kuwa ni Adelina Philimon (45) mkazi wa kijiji cha Magamba kata ya Magamba wilayani Chunya akiwa na mwanaume Wasiwasi Mwashiombo (28)  mkazi wa Ipoloto wilayani Mbozi.

Alisema nyumba hiyo inadaiwa kuchomwa na Zacharia Joseph Mkazi wa Tunduma wilayani Momba baada ya kuhisi marehemu hao wapo ndani ya nyuma.

Alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya kumkuta mpenzi wake akiwa na mwanaume mwingine ndani na amelalanae.

Mayala alisema kuwa katika tukio la pili ambalo lilitokea majira ya saa 20:00 usiku katika maeneo ya Mpona kata ya Totowe wilayani Chunya mkoani hapa ambapo mtu mmoja aliuwawa na watu wawili ambao hawakufaamika jina kabla na wao kuuwawa na wananchi wenye hasira kali.

Akisimulia tukio hilo Mayala alisema kuwa Jampany Mhamali (78) Mkazi wa Mkazi wa kijiji cha Mpona aliuwawa na watu wawili wasio fahamika majina ambao wali mjeruhi kwa mapanga mzee huyo Kichwani na mkono wake wa kulia baada ya kumkuta njiani akielekea nyumbani akitokea katrika kilabu cha pombe.

Wananchi wa maeneo hayo baada ya kugundua kifo cha mzee huyo ambaye aliuwawa kwa tuhuma za kishirikina walifuatilia walikoelekea wauwaji hao na kuwakamata kisha kuwauwa kwa mawe baada ya kuwatajia aliye watuma kumuuwa mzee Mhamali.

Kabla ya kuuwawa wauwaji hao walisema kuwa walitumwa na Maneno Adamson mkazi wa maeneo hayo ambaye alitoroka mara baada ya tukio hilo na jeshi la Polisi lina endelea kumtafuta mtuhumiwa huyi na miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwambani wilayani Chunya.