WANASANSI WATAKAO FAURU KUFADHILIWA





  • Ni kauli ya Mkurugenzi wa Wiza Sekondari ya Mbozi, Mbeya
  • Kumi watakaofanya vizuri kulipiwa ada miaka ya masomo
  • Apania kuisaidia serikali kufikia marengoi ya BRN 'Big Result Now'

JAMII Nchini imetakiwa kujitolea kuchangia kusomesha watoto wenye ufauru wa masomo ya sayansi ili nchi ipatekuwa na wanasayansi wengi hapo baadae.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Ileje Rosemary Sinyamule katika maafari ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Wiza ya Wilayani Mbozi Mkoani hapa yaliyofanyika mwishoni mwa Wiki iliyopita shuleni hapo.

Sinyamule alisema kuwa watoto wanaosoma masomo ya Sayansi wapewe motisha kwa kupewa udhamini wa masomo yao ili kuwashawishi na watoto wengine ambao walikuwa hawapendi kusoma somo hilo ambalo linabeba wataalamu mbalimbali na nchi yetu ikiwa na uhaba wa wataalau hao.

Alisema kwa kufanya hivyo serikali ipapata wataalamu wakutosha katika kila sekta hapa nchini na kuacha kutumia wataalamu kutoa nje ya nchi.

Aliyasema hayo muda mfupi baada ya kusikia kutoka katika risala ya iliyosomwa na mkuu wa shule hiyo ikilenga kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi 10 watakao fanya vizuri katika masomo ya sayansi.

Hivyo Sinyamule aliwataka wazazi wajitahidi kuwasomesha watoto wao na wale wenye uwezo kujitolea kuwasaidia wanafunzi ambao wanashindwa kulipa ada zashule na wanauwezo katika masomo yao ili kuinua elimu hapa nchini.

Awali akisoma risala kwa mgeni rasimi mkuu wa shule ya Wiza Simon Kibona alisema kuwa uongozi na bodi ya shule hiyo imelenga kuwasaidia wanafunzi 10 wanakao fanya vizuri katika masomo ya sayani kwa kuwalipoa ada katika msimu wote wa masomo yao.

Alisema kuwa watasaidia wanafunzi hao kwa muda wao wote wa masomo wawapo kidato cha tano na sita ili kupata wataaramu mbalimbali kwa wingi.

Nae mkurugenzi wa shule hiyo Charles Chenza alisema kuwa watatoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi watakao fanya vizuri ili kuisaidia nchi katika mikakati yake ya kufikia matokeo makubwa sasa ‘Big Result Now (BRN)’ katika sekta ya elimu.

Alisema kuwa kufatia juhudi zilizo wekwa na shule hiyo kufikia ma\lengo ya serikali wanajitahidukufundisha na katika mdihani wa kujiandaa na mtihani wa taifa shule hiyo imehika nafasi ya name kati ya shule 267 za mkoani Mbeya.