Barozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhart |
WATU wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi wapo
katika mazingira magumu ya kupatwa na
Ugonjwa wa Kifua kikuu hapa nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maabara
ya Kifua kikuu ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya, barozi wa
Marekani Nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt, jana alisema kuwa watu wanaoishi na
Virusi Vya Ukimwi wapo hatarini kupata ugogonjwa wa Kifua kikuu.
Alisema kuwa ili kupambana na kupiga
vita Kifua kikuu hapa nchini watu wa Marekani wameamua kujenga maabara itakayo
kuwa ikipima na kutoa tiba ya Ugonjwa huo.
Alisema kuwa watu wanaoishi na virusi
vya Ukimwi wapo hatarini kupatwa na ugonjwa wa Kifua kikuu na kuwa katika
hatari ya kufa mapema.
Add caption |
“Maabara hii ambayo sisi tumesimamia ni
muhimu katika kupiga vita dhidi ya Ukimwi na Kifua Kikuu nchini Tanzania na
hasa wananchi wa Nyanda za Juu Kusini” alisema Lenhardt.
Alisema kuwa Kifua Kikuu kinachochea
maendeleo ya ugonjwa wa Ukimwi kwa mtu anayeishi na Virusi vya Ukimwi na
kupelekea mtu huyo kufikwa na maupi mapema.
Lenhardt
alisema kuwa maabara hiyo itasaitia utambuzi wa haraka wa ugonjwa wa kifua
kikuu kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Vifusi vya Ukimwi na kuwakinga na
kifua Kikuu.
Alisema hapo awali ugonjwa huo ulikuwa
ukigunguliwa wakati wa matibabu ya ndio ulipo kuwa ukigundulika kwa mgonjwa na
ukiwa umemuadhiri sana mgonjwa.