KYELA VIJANA 20 WAPATIWA MAFUNZI




KAMPUNI inayojihusisha na ununuzi wa zao la Kakao Wilayani Kyela Mkoani Mbeya ya Olamu Tanzania Limite limetoa mafunzo ya matumizi yaumwagiliaji wa dawa mashambani kwa vijana 20 kutoka kata mbalimbali wilayani humo.

Akizungumza na wandishi wa habari Ofisini kwake Meneja wa Kampuni hiyo Wilaya ya Kyela Godfrey Okungu alisema kuwa kutokana na vijana wengi kujiingiza katika kazi za kumwagiia dawa mashambani kama moja ya kujipatia kipato chao bila kuzingatia sheria za matumizi ya dawa hizo kampuni iiamua kuwapa mafunzo mafupi.

Okungu alisema kuwa mafunzo hayo yalilenga zaidi katika uhalisia wa namna ya kutumia dawa hizo, muda wakupiga, kiasi cha dawa
kinachotakiwa kwa kuzingatia ukubwa wa shamba.

Alisema kuwa awai vijana hao walikuwa wakipiga dawa bila kuangalia upepo unatoka wapi na unaelekea wapi pasipo kutumia vifaa vinavyoweza kudhibiti dawa ii zisiwadhuru.

“kwa kutambua umuhimu wa vijana hao kampuni iiona kuwa vijana hao ni moja wa wadau wetu kwa wakuima hivyo tuiamua kuwapatia mafunzo ya matumizi ya dawa nakuwapelekea vifaa vya kuvaa wakati wa kupiga dawa shambani”alisema Okungu.

Alisema kuwa vifaa ambavyo kampuni yake iliwapatia vijana hao ni pamoja na Gamputi, Ovololi Gloves, Maski, na Miwani ya jua ambapo kia mmoja wao aipata kwa ajii ya kujikinga na dawa.

Aliongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa wakulima kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya matumizi ya dawa hizo na uwepo wa aina tofauti wa dawa hizo hivyo kupeekea wakuima kuendeleza mfumo wa kizamani wa namna ya upigaji wa dawa mashambani.

Aidha alisema kuwa suala la uelimishaji jamii au wakulima lisiwe la serikali tu, bali kila mmoja anapaswa kulitambua na kutoa elimu kwa wale ambao hawajaifikiwa ili kunusulu maisha ya wananchi kutokana na


matumizi mabaya ya dawa hizo.