JAMHURI KIHWELO KUPELEKWA MAHAKAMANI KWA KUTISHIA MAISHA YA MCHEZAJI

KIUNGO wa Toto African ya Mwanza, Emmanuel Swita amesema anajipanga kwenda Mahakamani kwa ajili ya kumfungulia mashtaka, kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' kumtishia maisha.

Uamuzi wa nyota huyo wa zamani, Kahama United na Yanga umekuja baada ya kocha Julio kudai alimpiga ngumi ya jicho baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kati ya Simba na Toto Uwanja wa CCM Kirumba juzi Jumamosi na kusisitiza kutoondoka Mwanza hadi atakapolipa kisasi.


Ugomvi wa wawili hao ulianza mara baada ya kocha Jamhuri Kiwhelo kudokezwa na mashabiki uwanjani hapo kuwa mchezaji huyo amechukua mpira uliodaiwa kuwa ni mali ya klabu ya Simba.



Julio baada ya kupata habari hizo alipanda kwenye gari la Toto African na kuchukua ufunguo wa gari kushinikiza gari hilo halitaondoka hadi mpira huo utakapopatika.


"Kweli nilikuwa na mipira ambayo ni mali ya timu ya Toto kuiweka kwenye gari. Nadhani ni kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuhisi ni mimi niliyechukua mpira wa Simba."


"Julio alivyopanda kwenye gari alichukua ufunguo kwa dreva kuzuia gari isiondoke huku akitupiana maneno na wachezaji."


"Kwa suala la kumpiga ngumi sijui aliyempiga. Nimesikia akinishutumu kwenye vyombo vya habari kuwa mimi ndiye niliyempiga na kunitishia maisha."


Swita alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa ameongea na viongozi wa timu yake kwa ajili ya kumfungulia mashtaka Julio kumtishia amani na kumuunga mkono kwa uamuzi huo.


"Tarifa ambazo nimesikia akitangaza kwenye radio ni kwamba hataondoka Mwanza mpaka atakapolipa kisasi."


"Kwa hiyo, ili kujiweka katika hali ya usalama na hilo naenda kukata 'RB' na viongozi wangu wameniahidi kunipa ushirikiano wa kutosha." alisisitiza mchezaji huyo.


Chanzo Shaffih