WIZARA IBORESHE HUDUMA ZA MAJI NA KUONGEZA WATEJA
WIZARA ya maji safi na maji taka mkoani mbeya imetakiwa kuongeza zaidi
wateja, ili kuboresha ufanisi wa huduma ya maji hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa Juzi jijini Hapa na Mstahiki Meya wa Jiji la
Mbeya Mh. Athanas Kapunga Kwenyesherehe za kilele cha wiki ya maji
Kitaifa ambayo kimkoa yalifanyika jijini Hapa katika ukumbi wa Parokia
ya kanisa Katoliki.
Mh. Kapunga ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo, alisema
kuwa pamoja na kwamba maji ni uhai lakini yanahitaji utunzaji bora kwa
afya za binadamu.
Alisema kuwa japokuwa kaulimbiu inasema kuwa ‘Huu ni mwaka wa
ushirikiano wa maji kitaifa,’ lakini inatoa funzo juu ya utunzaji bora
wa maji.
Kapunda alisema kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Bw. Jumanne Idd
amepewa jukumu atilie mkazo wa utunzaji wa maji safi, ili wananchi
waweze kupatiwa huduma iliyo bora.
Mstahiki Meya huyo wa Jiji aliongeza kuwa Jiji likikosa maji kwa masaa
kadhaa wananchi watapata shida katika matumizi yao mbalimbali ya kila
siku na kazi itaharibika.
Alisema pia kuwa ili wafanyakazi wa idara ya maji wafanye kazi kwa
bidii wanatakiwa kutokuwa na vinyongo na pia wapunguze manung’uniko.
Awali Mkurugenzi wa idara ya maji safi na maji taka jijini Mbeya,
Mhandisi Simeon Shauri akisoma risala kwa mgeni rasimi aliitaka wizara
kuongeza zaidi idadi ya wateja, na kuwahimiza wafanya kazi kuchapa
kazi kwa bidii ili kuboresha huduma za kazi.
Hivyo mkurugenzi huyo wa maji aliwataka wafanyakazi idara hiyo
waongeze bidii zaidi katika kazi zao, ili kuweza kulitandaza vyema
jiji la Mbeya.
Mwisho