MTU mmoja mkazi wa Kijiji cha Mbebe
Wilayani Ileje Mkoani Hapo Wilson Mlwafu (68) ameuawa kwa kukatwa na upanga
sehemu mbalimbali za mwili kwa tuhuma za ushilikina.
Tukio hilo limetokea limetokea
February 2 mwaka huu majira ya saa 3:30 usiku ambapo marehemu alikuwa anatoka
kirabuni kunywa pombe za kienyeji na kukutana na kundi la vijana walio anza
kumshambulia.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary
Senyamule alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu huyo
alikuwa anatuhumiwa na watoto wake kuwa anafanya mambo ya kichawi jambo ambalo
halina uhakika.
Rosemary alisema kuwa serikali ya
Tanzania haiamini masuala ya kishirikina hivyo aliwataka wananchi
kutokujichukulia sheria mkononi na kudai kuwa iwapo mtu atabainika kufanya
hivyo sheria zitachukuliwa juu yake.
Serikali yetu haiamini masuala
ya uchawi na kuwa watu wamekuwa wakisema mara kwa mara kuhusu uchawi na mambo
yanatokea ya mauaji kwa wingizaidi na tumekuwa tukishuhudia watu wakiuawa kwa
tuhuma kama hizo za ushrlikina” alisema Senyamule.
Senyamule alisema kuwa marehemu
alikatwa na upanga sana sehemu za kichwani na kuwa alikufa papo hapo kwa kuwa
alikuwa amelewa pombe na watu waliofanya unyama huo walichukua nafasi hiyo ya
kumvamia na kumuua.
Alisesema wananchi waache kujichukulia
sheria mkononi kwa kufanya mauaji kama huyo na kuwa inatishia amani kwa
wananchi kuwa wanaweza kuuliwa pasipo kuwa na ukweli kwa madai kuwa ni
washirikina.
Mkuu huyo aliongeza kuwa
upelelezi unaendelea wa tukuio hilo kwa kuwa chanzo bado hakijafahamika vizuri
na kuwa jeshi la polisi linafanya kazi ya kuwatafuta walio fanya unyama huo na
kuwa wananchi watoe ushirikiano katika suala hilo.