MOSCOW : MAELFU WAANDANANA KUNPINGA PUTIN

Maalfu ya watu walijitokeza kwenye barabara za mjini  Moscow ili kufanya maandamano makubwa ya  kuupinga utawala wa Rais Vladmir Putin. 

Viongozi wa upinzani wamesema walioshiriki katika maandamano hayo walifikia watu laki moja, lakini polisi  imesema walioshiriki walikuwa watu 20,000 Polisi waliopambana na waandamanaji waliompinga   Putin mnamo mwezi wa Mei walikuwa katika hali ya  tahadhari lakini hawachukua hatua yoyote safari hii.

Maandamano yalifanyika kwa muda wa saa sita na  yalimalizika kwa amani . Maandamano hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza  tokea Rais Putin atie saini sheria mpya wiki iliyopita, ya  kuwezesha kuwapa watu adhabu ya kulipa faini kubwa  zaidi ikiwa wanashiriki au wanaandaa upinzani ambao haukuruhusiwa.