WAKAZI Nsenga na wa kijiji kipya cha Ilangali halmashauri ya Mbeya vijijini wametakiwa kushirikiana kuchangia michango ya madawati na ujenzi wa shule za msingi ili kuondoa migogoro ambayo ipo baina ya wakazi hao.
Hayo yalisemwa na katibu tarafa ya Swaya, Felix Lyaniva baada kutokuwepo maelewano ya moja kwa moja baina ya pande mbili kati ya wakazi wa vijiji viwili vya Nsenga na Ilangali juu ya uchangiaji wa michango ujenzi wa vyumba vya madarasa na uchangiaji wa madawati katika shule ya msingi Nsenga.
Lyaniva aliwataka wakazi wa Ilangali kuachana na malumbano ambayo hayana msingi wowote katika kukuza na kuendeleza taluma kwa wanafunzi wa Nsenga hali hiyo si shwari katika maamuzi ya wakazi wa Ilangali ambao walisema hawatakuwa tayari kutoa mchango wowote unaohusiana na shule ya msigi Nsenga kwa madai kwamba wao wanamzigo wa shule ya msingi Ilangali na si vinginevyo.
Mkutano huo uliohuzuliwa na viongozi mbalimbali wa tarafa na kata ukiongoza na Lyaniva aliyetoa rai kwa wananchi hao kuungana kwa pamoja kuleta maendeleo ya Nsenga na si malumbano.
"Ushirikiano ukiwepo katika jamii yoyote ya kitanzania tutasonga mbele katika shughuli za maendeleo kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu" alisema Lyaniva.
Alisema maendeleo ya shule hiyo huletwa na wazazi na sio serikali kama wanavyo dhani pia wamewataka wakazi wa Ilangali kuwa suala la ujenzi wa shule ya msingi Nsenga linawahusu wakazi wote na sio la wanansenga tu.
Pamoja na hayo yote kuliibuka mabishano kati ya mgeni rasmi na wakazi wa Ilangali waliodai kumalizika kwa mkutano huo hakujawapa jibu kamili la nani anatakiwa kuchangia madawati na ujenzi wa vyumba vya madarasa na Madawati ya shule ya msingi Nsenga mgeni rasmi alisema suala hilo atalifanyia kazi.