ASKOFU wa kanisa la kipentecostel -Mlima Sayuni Adamson Mwaisumo (Nabii) kutoka Nairobi ametoa tamko juu ya soko la Sido lililoteketea kwa moto mwishoni mwa mwaka 2011 kuwa liliungua kutokana na giza.
Aliyasema hayo hivi karibuni, katika mkutano wa injili uliyofanyika katika eneo la Uyole mkoani hapa kuwa soko hilo lililopo Mwanjelwa liliungua kwa sababu ya kundi dogo la watu linalojihusisha na ushirikina na kufanya maeneo ya masoko kama sehemu za mikutano yao nyakati za usiku.
Nabii Mwaisumo alisema ,kama watu watashindwa kukubaliana na usemi wake watafakari kwanini moto ulianza mdog lakini kundi kubwa la wafanyabiashara lilishindwa kuudhibiti mapema moto huo mpaka kufikia hatua kubwa huku wakibaki na mshangao.
Askofu alisema kuwa, ardhi ya nyanda za juu kusini imebarikiwa kuwa na mazao na ndiyo maana wanaochoma masoko lengo lao ni kutaka ardhi ilaaniwe iwe na ukame.
''Sumbawanga ,Iringa na Mbeya mikoa hii ardhi imebarikiwa ,mungu amesema na mimi kuwa wanajihusisha na ushirikina kutoka sehemu mbali mbali ili kuilaani ardhi hii kwa kuchoma masoko kupitia nguvu za giza,wakumbuke watumish tupo tutaomba mkoa huu utazidi kusonga mbele ''Alisema Mwaisumo.
Alisema tunatakiwa kutambua kuwa,kitendo cha kuchoma masoko ovyo ni kutaka ardhi ilaaniwe hivyo kila mmoja anatakiwa kuwa mwangalifu.
Alitoa wito kwa watumishi kutoa ushirikiano ili kuumbea mkoa wa Mbeya kutkana na matukio ya moto ambayo yalikithiri mwishoni mwa mwakajana kusudi yasijirudie tena.
HABARI LUJECO NA EMMY