MCHUNGAJI wa kanisa la Evangelist Asesemblies of God Tanzania usharika wa Galilaya Mbalizi jijini Mbeya, Ayub Mwasiposya jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na wananchi katika mkutano wa hadhara.
Mchungaji huyo alipata aibu ya kuzomewa na wananchi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika eneo la Tazara katika mji mdogo wa Mbalizi baada ya kupata nafasi ya kujieleza ni kuhusu taarifa alizo shiriki kuzipeleka kwenye ofisi ya mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya.
Habari zinasema kuwa, mchungaji huyo pamoja na wenzake wawili alipeleka malalamiko kuwa wananchi wa mtaa wa Tazara wananyanyaswa na mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Benson Mwakilembe na kudai kuwa wananchi hao wamefikia hatua kumtaka Mwakilembe ahame katika mtaa huo.
Habari zaidi kuhusiana na tukio hilo zinasema kwamba mchungaji huyo aliwaongoza wenzake kwa shinikizo la uchochezi wengine waliotajwa ni majina ya Cosmas Maluli na Chacha Mwita hadi kwenye ofisi za upelelezi mkoani na kueleza malalamiko hayo .
Taarifa kutoka ndani ya jeshi la Polisi mkoani hapa zinasema kuwa baada ya kupata taarifa hizo waliwasiliana na uongozi wa mtaa uongozi ambao ulikana kuwepo na tuhuma hizo na ulipendekeza ufanyike mkutano wa hadhara ili kuthibitisha tuhuma hizo mbele ya wananchi.
Katika mkutano huo ambao ulianza majira ya saa 11 za jioni ukihudhuriwa na mkuu wa kituo kidogo cha Polisi kilichopo Mbalizi ,Seleman Manyanga, viongozi wa serikali ya mtaa huo na wananchi wa eneo hilo ulishindwa kufikia muafaka baada ya RCO kushindwa kufika.
Baadhi ya watu waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi eneo la Tazara Mbalizi wamesema kuwa, chanzo cha mchungaji huyo kuzomewa kilitokana na yeye kujiingiza kwenye ugomvi na mfanyabiashara huyo kwa kipindi kirefu huku akimtuhumu Mwakilembe kujipatia mali kwa njia za kishirikina.
"Hakuna lolote ni wivu tu unao wasumbua baada ya mwenzao kubahatika kupata mali ambazo tunafahamu kazisotea kwa muda mrefu huko machimboni,"aliyasema mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina moja la Sanga .
Mwasiposya mnamo mwaka jana aliingia kwenye ugomvi mkubwa na Mwakilembe ambaye pia aliwa kuwa muumini wake, ugomvi huo ulimfikisha Mwasiposya Mikononi mwa polisi yeye na familia yake iliyofika kituo cha polisi Mbalizi na kufanya fujo muda mfupi baada ya Mwasiposya kukamatwa.
Akiwa mikononi mwa polisi ,Mwasiposya alifuatwa na watoto wake kwa kusudi la kujua kosa la baba yao hatimaye nao wakajikuta wako hatiani kama ilivyo kuwa kwa baba yao kufuatia vurugu zao.
Vile vile mchungaji huyo amelalamikiwa na baadhi ya wakazi wa vitongoji vya Chapakazi naMlimareli kwa madai kuwa mahubiri yake yamekuwa kero kwa wakazi hao kutokana na mchungaji huyo kuhubiri kwa sauti kubwa ya vipaza sauti usiku wa manane.
Akizungumza na mwandishi wahabarihizi nyumbani kwake mwenyekiti wamtaa wa Chapakazi aliyejitambulishakwa jinala Jacob Ntengule alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa wakazi wamtaa wake .
Ntengule alisema kwamba ,mahubirihayo yamekuwayakiharibu doria inayo fanywa na sungu sungu wamaeneo hayo.
Mchungaji Mwasiposya alipofuatwa nyumbani kwake ilikuelezea tukio hilo alikiri pamoja na kupokea onyo la kuhubiri usiku wa manane.
Balozi wa mtaa wa Chapakazi ameshauri kuwa serikali iingilie kati suala hilo kwa madai kuwa kunadalili mbaya ya uvunjifu wa amani.
Mwakilembe alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa amedhalilishwa sana na mchungaji wake na kudai kuwa ameishangaza jamii inayo mzunguka kwa udhaifu wa kiimani.