KUCHELEWA KULIPA MICHANGO NOMA


Baadhi ya wazazi kushindwa na kuchelewa kutoa pesa kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Ilomba iliyopo jijini Mbeya kunapelekea kuzolota na kuchelewa kukumilika kwa zoezi hilo .

Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji Bw . PYUSI MOSES alipokuwa katika mahojiano na rock fm na kusema kuwa wazazi kushindwa na kuchelewa kutoa pesa kunarudisha nyuma ujenzi wa vyumba vya madarasa .

Pia  amesema serikali na wazazi kwa pamoja walipanga kufikia tarehe 5 februali  wawe wamakamilisha zoezi la utoaji fedha kiasi cha shilingi elfu (5000 ) kwa kila mzazi lakini zoezi hilo halikufanikiwa na kueleza kuw aserikali imeamua kuongeza muda mpakankufikia tarehe 10 (April) kila mzazi awe amatoa pesa hiyona kuongeza kuwa atakaekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Mbali na hayo Bw PYUSI ameataka wazazi kuwa na mwamko katika suala la Elimu ili kuleta maendeleo ya Taifa na kjenga misngi mizuri kwa kizazi cha sasana cha Baadaye.