AFUKUZWA SHULE KWA KUPEWA MIMBA


Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Iwalanje, halmashauri ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya Pendo Jacob (17), amepoteza amefukuza shule baada ya kubaainika kuwa ana mimba ambayo amepewa na mwanakijiji.

Pendo amebainika kuwa ana mimba aliyopewa na Bw. Shungu Ringston Ndasoni (28), mkazi wa Kijiji cha Hatwelo, Kata ya Iwalanje ambaye ni alikuwa na uhusiano nae wa kimapenzi.

Mwanafunzi huyo amefukuzwa shule hivi karibuni kufuatia wazazi wake Bw. Jacob Mwakambanga (60), kuitwa na Mkuu wa shule na kuambiwa kuwa binti yao ana ujauzito wa miezi minne, baada ya kupimwa katika Zahanati ya kijijini hapo.

Wazazi wake wamepewa barua ili wawakaisaini kwa afisa mtendaji ili kufuatataratibu za kufutajina la mwanafuzi huyo shuleni.

Aidha, Bwana Yassin Yuta (32) ametishiwa na viongozi hao na kumzuia asiendelee kufuatilia mambo ya kijiji hicho, baada ya kuonekana mnamo Aprili 17 mwaka huu akiwa na waandishi wa habari baada ya kumshutumu kutoa siri za kijiji hicho kwa vyombo vya habari na kishi kumuoanya kucha mara moja vinginevyo wanamuua.

Kufuatia sakata hilo ukaitishwa mkutano wa hadhara, siku hiyo hiyo na kusimamiwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Mponzi na kutoa agizo kuwa Bwna Yassin asionekane katika kijiji hicho na kuwamuru wananchi wakimuona wachukue sheria mkononi au kuuawa.