AFISA MTENDAJI ATIMULIWA

WAKAZI wa kijiji cha Mpangala kata ya Halungu wilayani Mbozi wamefunga ofisi ya afisa mtendaji na mwenyekiti wake baada ya kutoa taarifa ya kata hiyo ambayo haikua sahihi.

Wakizungumza na NIPASHE na wakazi hao wamedai kuwa afisa mtendaji ambeye alifahamika kwa jina moja la Mkondya pamoja na Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Musa Mkondya wamefukuzwa katika kijiji hicho kwa kufunga ofisi zao kwa madai ya kutokusoma mapato na matumizi sahihi ya kijiji hicho.

Walisema voongozi hao walisoma mapato na matumizi yasiyo sahihi na kuvyo yamewakeli kiasi cha kufunga ofisi zao.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Samson Simkoko amejaribu kuzungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika jana lakini jitihada hizo zilishindikana kutokana na wananchi kuwekea mkazo wa kutowahitaji katika kijiji hicho.

"Licha ya mimi kuitisha mkutano wa kuzungumza nao lakini wamegoma kabisa viongozi hawa kuludi katika ofisi zao" alisema  Simkoko

Hata hivyo mpaka mwisho wa mkutano huo hitimisho haikuweza kufikia na diwani aliamua kuondoka na afisa mtendaji pamoja mwenyekiti na kuazimia kuleta afisa mtendaji ambaye kaimu nafasi Mkondya mpaka pale mambo yatakapokaa sawa.

"Mambo yakikaa sawa watarudi kazini lakini kwa sasa watatafutwa watu wawili watakao kaimu nafasi zao kwa muda hadi hapo baadae" aliongeza  Simkoko.