KIMATAIFA

  • Ni jumanne ya uchaguzi wa urais Yemen

  •  YEMEN KUINGIA UCHAGUZINI LEO
Raia wa Yemen wanaamkia katika vituo vya kupigia kura kumchagua rais wao mpya, leo Jumanne.

Wafuasi wa Abd Mansour Hadi katika kampeni

Lakini kila mtu anajua kuwa atakayeshinda ni makamu wa Rais Abd Rabbu Mansour Hadi.
Yeye ni mgombea wa pekee. Hana mpinzani.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya mwaka mmoja wa ghasia na maandamano ya kupinga utawala wa Rais Ali Abdullah Saleh.
Kampeni zimekuwa zikiendelea kumuunga mkono makamu wa rais Abd Rabbu Mansour Hadi.
Mshindi wa tuzo ya Nobel raia wa Yemen Bi Tawwakol Karman amewataka raia wote wa Yemen kujitokeza kumuunga mkono Makamu huyo wa Rais, Bwana Hadi.
“Tunawaumba watu wote wa Yemeni wakiwemo vijana wajitokeze hii leo tarehe 21 Februari, sio kuunga mkono uchaguzi peke yake, bali kumuunga mkono Masour Hadi kuwa Rais wa mpito katika kipindi hiki cha mpito”,Bi Karman amesema.
Huku Mshindi huyo wa Tuzo ya Nobel akimpigia debe Bwana Mansour Hadi ghasia zimeanza upya nchini Yemen.
Pia kumeripotiwa mfululizo wa milipuko na mashambulio katika vituo vya kupigia kura na sehemu nyingine


Jeshi la Nigeria lawauwa Boko Haram


Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kwamba wanajeshi watatu walijeruhiwa katika
makabiliano hayo ya risasi na kundi la Boko Haram.
Walinda usalama katika mji wa Maiduguri


Taarifa zinazohusiana

Hata hivyo alikanusha kuwa kuna raia yeyote aliyeuwawa katika kisa hicho.
Lakini wenye maduka katika soko la Baga wamenukuliwa wakisema kuwa wameona maiti zipatazo ishirini hivi zikipakiwa kwenye lori.
Eneo hilo la Maiduguri ni ngombe kuu ya wapiganiaji wa Boko Haram . Na katika miaka ya hivi karibuni sehemu imeshuhudia milipuko kadhaa na ufyatuliananji wa risasi.
Tayari serikali ya rais Goodluck Jonathan imetangaza hali ya hatari katika mji huyo na miji menginea ambayo imeshuhudia mashambulizi toka kwa kundi hilo la Boko Haram.
Lakini wakazi wa miji hiyo wanasema kuwa suluhu ya kijeshi haijafaulu leta mafanikio yeyote