Watu watano wamefariki dunia katika matukio matano tofauti, yakiwemo matatu yanayohusishwa na ajali za barabarani mkoani Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoani mbeya Advocate Nyombi amesema Benardi Bakinga (32), mkazi wa Ilomba Jijini Mbeya ameuwawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kujihusha na wizi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hosipitali ya Rufaa jijini hapa na mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo .
Aidha Nyombi ameongeza kuwa tukio jingine lili tokea katika kijiji cha Masebe wilayani Rungwe ambapo Helodi Mwakesesya (56) mkazi wa kijiji hicho ameuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumtuhumu marehemu kujihusisha na imani za kishirikina.
Jeshi lapolisi linawashikilia watu wawili ambao ni Zacharia Mwauibinga (30) na Zaward Emmanuel (30) wote wakiwa wakazi wa kijiji cha Masebe ambapo wanatuhumiwa kutenda kosa hilo majira ya saa tano usiku Februari 20 mwaka huu.
Chanzo cha mauaji hayo ni kile kilichodaiwa marehemu alikuwa akijihusisha na imani za kishirikina na kabla ya kufanya mauaji hayo nyumba ya marehemu ilichomwa na moto.
Kamanda Nyombi ameongeza kuwa Essau Kiswaga (22) amefariki baada ya gari aina ya pikipiki yenye namba za usjili T255 APR kupinduka na kusababisha kifo chake tukio hilo lilitokea Februari 20 katika barabara ya Mbeya - Iringa ambapo gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Deodatusi Neumwa (36) ambaye ni mkazi wa Mafinga na kupinduka katika kijiji cha Uinyagogwa huko Madibila wilayani Mbarali.
Chazo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendokasi na Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa gari hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Na katika tukio lingine jijini Mbeya katika eneo la Mwanji barabara ya Mbeya - Iringa gari lenye namba za usajili T 642 AED Toyota Hiace lililokuwa likiendeswa na dereva aitwaye Laightoni Frolence (25) mkazi wa Ilomba jijini Mbeya ilimgonga mpanda pikipiki yenye namba za usajili T 127 BUV aitwaye Tidibows Mwakatowe (30) na kusababisha kifo chake papo hapo na abiria wake KERVINI NDONDE mkazi wa ILOMBA jijini hapa kupatwa majeraha .
Mwili wa mrehemu umehifadhiwa kastika Hospitali ya Rufaa jijini hapa na majeruhi wote wamelazwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari na pikipiki vyombo hivyo vipo katika kituo cha polisi jijni humo
Wakati huo huo Geophrey Mwankenja amefariki dunia baada ya kugongana uso kwa uso na gari aina ya Hiaceakiwa kwenye pikipiki na abiria aitwaye Njala Mwankulu ambaye aliyelazwa katika hosipitali hiyo.
Ajali hiyo imetokea baada ya pikipiki hiyo kujalibu kuli pita basi la FALCON majira ya saa kumi za jioni na hivyo kukutana uso kwa uso na HIACE na kufariki papo hapo.