Mkurugenzi wa taasisi ya kusaidia watoto walemavu Child Support tanzania iliyopo Block T jijini Mbeya Bi Noela Msuya ametoa wito kwa jamii kutowatenga na kuwaficha watoto wenye ulemavu.
Hayo yamesemwa na Bi Msuya alipokuwa akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake amesema jamii inatakiwa kuwashirikisha na kuwawezesha walemavu katika mambo mbalimbali ya maendeleo katika jamii
Aidha ameongeza kuwa watoto walemavu ni sawa na watoto wengine na wana uwezo ,vipaji pia jamii inatakiwa kuviendeleza vipaji ili wasije kuwa tegemezi kwa maisha ya baadae.