TANZANIA PRISONS YAPANIA KURUDI LIGI KUU TANZANIA



MABINGWA  wa ligi ya muungano Tanzania kwa mwaka 1999 Tanzania Prisons ya Mbeya, wamepania kurudi katika ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao ili kulinda heshima ya mkoa wa Mbeya.

Kauli hiyo imetolewa na hivi karibuni na mmoja wa wachezaji wa timu hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina kwa vile sio msemaji wa timu, wakati alipozungumza na RAHATELE jijini Mbeya.

Prisons ni miongoni mwa timu tatu kutoka kundu ‘B’ zilizo fuzu kucheza hatua ya tisa bora baada ya kuu msimu ujao ni polisi morogoro, Rhino na Polisi FC zote kutoka mkoani Tabora.

Prisons ambayo ilipanda daraja mwaka 1995 na kucheza ligi kuu mwaka 1996 ni moja kati ya timu machachari kutoka mkoani Mbeya zilizo kuwa zikifanya vizuri, na kutoa upinzani mkali kwa vigogo vya soka hapa nchini vya Simba na Yanga, pamoja na timu zingine.

Timu zingine kutoka hapa jijini ambazo kwa sasa hazipo tena katika ulimwengu wa soka ni Tukuyu Star (Banyambala) iliyo twaa ubingwa mwaka 1986 baada ya kupanda daraja mwaka huohuo, Mecco FC, Tiger FC ya Tunduma na 44 KJ zote zilikuwa za mkoa wa Mbeya.

Timu hiyo ilichukuwa ubingwa wa ligi ya muungano mwaka 1999 ikiwa na wachezaji mahiri kama vile makipa Amani Simba, Ivon Mapunda na Dennis Edwin.

Wengine ni Samson  Mwamanda Hussein  Mataka, Primus  Kasonso, Havinitishi Abdallah, Nseka Bugoya, Athuman Mwagwego na Victor Kilowoko.

Wachezaji wengine ni Oswald Morris, Gerald Hillu, Munyu Kassm, Daudi Kufakunoga, Nassib Tondogoso, Hassan Mutego na Hemed Mrisho chini ya kocha mkuu Charles Boniface Mkwasa (Master), na msaidizi wake Freddy Felix Kataraia Minziro.

Mkuu wa chuo cha Ufundi cha magereza Ruanda Mbeya ambaye pia ni mlezi wa timu hiyo Mashaka Msote hakuweza kupatikana alipopigiwa simu na RAHATELE, ili aeleze kuhusu maendeleo ya maandalizi ya timu yake katika hatua ya tisa bora.

Prisons ili shuka daraja mwaka 2010 na tokea wakati huo mkoa wa Mbeya umekosa burudani ya michezo ya rigi kuu ya soka Tanzania bara, na kuishia tu kuwa msikilizaji kwenye redio na kutazama kwenye luninga.

Mwisho
kujikusanyia pointi 14, nyuma ya JKT Mlale yenye pointi 16 na Mbeya City iliyoongoza kundi hilo  kwa kupata pointi 22.

Timu nyingine zilizo fuzu kucheza hatua ya tisa bora ni Trans Camp na Polisi zote kutoka jijini Dar es salaam, pamoja na timu ya Mgambo JKT kutoka Mkoani Tanga.

Kutoka kundi ‘C’  timu zilizo fanikiwa kutinga hatua hiyo ambapo timu tatu za mwanzo zita panda Daraja na kucheza ligi