JAMII ITETEE WATU WENYE ULEMAVU


JAMII nchini imetakiwa  kutoa fursa sawa kwa watoto wenye ulemavu  katika mambo mbalimbali ya kijamii ili kuwapunguzia msongo wa mawazo  na dhana ya kwamba wanabaguliwa na jamii kutokana ulemavu walionao.


Akizungumza katika kikao mwezeshaji wa semina hiyo, Mwanasheria GIDION MANDESI amesema kumekuwa na utengano mkubwa baina ya watoto wenye  ulemavu na wasio na ulemavu  hali inayopelekea watoto hao kuonekana kama wametengwa na jamii katika ushilikishwaji wa mambo mbalimbali ambayo wana haki kuyapata.

Amesema kuwa yapo mambo kadhaa ambayo mlemavu amekuwa akionekana kubaguliwa kama kushiriki katika kuchangia mawazo yao bila kupingwa kutokana na ulemavu wake.

MANDESI amesema kuwa katika mkataba wa kimataifa juu ya haki ya mtoto  ya mwaka 1989 inasema kila mtoto mwenye ulemavu anatakiwa kupewa haki za msingi kama watoto wengine na sio kuwatenga.

Nae NICOLAUS MTAMBI ambaye ni  katibu tawala msaidizi mipango na utawala Mkoa wa Mbeya, amesema kuwa serikali inaunga mkono harakati hizo na kushirikiana na wadau mbalimbali ili kufanikisha azma ya serikali kuwekeza kwa watoto kwa mstakabali wa Taifa