USAJILI WASUMBUA WATAKA MPAKARUSHWA



USAJIRI wa waganga wa tiba asili na watabibu umekuwa unavikwazo mbalimbali katika ngazi za mtaa ambako wanatakiwa kuanzia kujisajili baada ya kuchukua fomu zao za usajili kutokana na watendaji wa mitaa kuwadai pesa za kikao chan kujadili usajili.

Hayo yalibainishwa katika kikao cha watabu na wakunga wa jadi wiki liliyopita wakati wakijali nini kifanyifike kuepukana na kashifa wanazotupiwa vitendo viovu vinavo tokea katika jamii hasa vile vya upigaji nondo.

Akizungunzia suala la usajili Mratibu wa chama cha ATME, Boniventura Mwalongo, alisema katika hatua ya usajili mganga hatotozwa kiwango chochote zaidi ya shilingi 35,000 au 55,000 kama ada ya usajili na si vinginevyo.

Alisema kama mganga atadaiwa pesa hiyo itakuwa ni Rushwa na hicho kimekuwa ni kikwazo kwa watabibu wengi kujisajili hasa walio vijijini.

Mwalongo pia ailisema kuwa si kazi ya mganga anayetaka kujisajili kufuatilia katika kila ofisi kujisajili na huduma hiyo.

 “kwa mganga anayejisajili ni kosa kufuatilia yeye menyewe katika ofisi za mtaa na hata katika ofisi za kata huo ni wajibu wa watendaji kusogeza mbele fomu yako baada ya kilizika katika ofiyi ya mtaa na kata hadi taifa,” alisema  Mwalongo

Mwalogo alisema fomu ya usajili itajadiliwa ndani ya mwezi mmoja katika ngazi ya mtaa na kusogezwa katka ngazi ya kata ambapo itajadiliwa ndani ya miezi mitatu kasha kusogezwa katika ngazi ya wilaya halikadhalika katika ngazi ya taifa.

 Baada ya hapo muhusika atapatiwa cheti cha usajili kama itapitishwa katika kilangazi bila kikwazo cheti hicho kitatolewa cha muda mfupi ambapo atakuwa katika kipindi cha miaka mitatu kama hata husika na makosa ya jinai kwa kipindi chote hicho aatapata cheti cha kudumu.

Kutokana na usajili huo kuwa mgumu vyeti nanekati ya hivyo vinne vilitolewa kwa waganga wa Mkoa wa Mbeya.

Kuhusiana na waokuhusika na maovu katika sehemu mbalimbali hasa yale ya mauaji ya watoto, albino na upigaji nondo wamesema hawahusiki walisema maovu hayo yanatokana na baadhi ya watanzania kukosa ajira na kazi zakufanya na kisha kusababisha kujiingiza katika mambo maovu.

Moja kati ya watabibu hao aliweka bayana kuwa wanao watuma watu hao kupiga watu nondouchunaji wa ngozi ingawa umepungua, mauaji ya watoto nay ale ya albino ni watu kutoka nje ya nchi ndio wanajitokeza katika nchi yetu na kuwalipa vijana kwa kazi hiyo.

Kutokana na uchunguzi alio ufanya alisema kuwa malango yao yamekuwa hasa katika mkoani Mbeya katika wilaya za Mbozi na Ileje na ndio maana ndiko kulivuma sana katika masuala ya uchunaji Ngozi.

Mwalongo alichukua nafasi hiyo kuwataka  wananchi kutofautisha kati ya wakunga wa jadi, watabibu na waganga wa  kienyeji wale wapigao lamri.

Mwisho