Wapiganaji wa Alshabab wapata pigo kubwa baada ya mji wa Baidoa kukombolewa na viksi vya Amisom.
Kuanguka kwa Baidoa kunafuatia shambulizi la majeshi ya tume ya Umoja wa Afrika huko Somalia (AMISOM) kulikotokea katika siku hiyo hiyo ambayo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kuongeza idadi ya vikosi hivyo kwa takriban wanajeshi 6,000.
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice amesema kura hiyo ya siri ya baraza hilo inaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kuvunja nguvu za kigaidi na kuleta amani.
Wawakilishi wa zaidi ya serikali 40 na jumuiya ya kimataifa wanakutana Uingereza kwa siku moja Alhamis kwa lengo la kuanzisha serikali thabiti huko Somalia. Nchi hiyo ya pembe ya Afrika haijawa na amani kwa zaidi ya miongo miwili.