KAMPUNI ya Misha Communication inatarajia kuendesha ligi ya Raha tele ya Mchangani itakayo zijumuisha jimu zaidi ya 20 za madaraja ya chini ya jijini Mbeya.
Ligi hiyo inayo tarajiwa kuwa na msisimko mkubwa itaanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao, katika viwanja vya shule za msingi za Mbata na Itiji zote za jijini hapa.
Mratibu wa ligi hiyo David Mwakalinga aliiambia RAHATELE Mwishoni mwa wiki jijini hapa kuwa, mashindano ya ligi hiyo yataanza nara baada ya kumalizika kwa ligi nyingine ya mwambambe ambayo inaendelea kuchezwa katika viwanja hivyo hivi sasa.
Mwakalinga alisema kuwa mashindano hayo yatadhaminiwa na kampuni ya Misha Communication ltd, ambao ni wachapishaji wa gazeti la michezo na burudani la RAHATELE.
Alisema kuwa timu zitakazo shiriki katika ligi hiyo zote ni za kutoka mbeya mjini, na kuongeza kuwa idadi kamili ya timu zitakazo shiriki katika mashindano hayo itatangazwa baadaye.
Mdau huyo wa soka alisema kuwa jingo kuu la mashindano hayo ni kuinua vipaji vya vijana chipukizi vilivyo fichika mkoani Mbeya ili viweze kuendelezwa kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa soka.
Mashindano hayo pia yata tungiwa sheria ndogondogo za kuendeshea utaratibu mzima wa ligi hiyo iliyaweze kuboreka zaidi, ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji kutoka shule za msingi na sekondari kwa manufaa ya mkoa wa Mbeya na taifa Kwa ujumla.
Wakati huohuo kikao cha maandalizi ya mashindano ya ligi hiyo kitafanyika leo saa 9:00 alasili, katika ukumbi wa bar ya Tugelepo iliyopo eneo la Ghana karibu na shule ya msingi ya Mbata jijini Mbeya.
Mwisho