Showing posts with label kilimo Afrika. Show all posts
Showing posts with label kilimo Afrika. Show all posts
 Msumbiji: Hatuna washukiwa waliomuua Karegeya

Msumbiji: Hatuna washukiwa waliomuua Karegeya


Kareguya aliuawa nchini Afrika Kusini huku Rwanda ikisema alikuwa adui wake
Polisi nchini Msumbuji wamekanusha madai kuwa wamewakamata watu wanaoshukiwa kumuua mkuu wa zamani wa ujasusi nchini Rwanda Patrick Karegeya.
Msemaji wa polisi nchini humo Joao Machava amesema kuwa hakuna mshukiwa aliyezuiliwa kuhusiana na mauaji hayo ya Patrick Karegeya ingawa kuna raia kadhaa wa Rwanda waliokamatwa nchini humo.
Awali alinukuliwa akisema wanyarwanda kadhaa wamekamatwa na wanatarajiwa kurejeshwa nchini Afrika Kusini.
Marehemu Karegeya alikimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini na alipatikana akiwa amefariki katika hoteli yake mjini Johannesburg January tarehe moja.
Polisi wanaamini kuwa Karegeya aliuawa.
Na BBCSwahili.
TEKNOHAMA kuinua kilimo Afrika

TEKNOHAMA kuinua kilimo Afrika

Imeelezwa kwamba ili bara la Afrika liwe na uhakika wa kujipatia chakula kwa ajili ya kuwalisha wakaazi wake, linahitaji kupiga hatua za haraka katika matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA).
Kilimo nchini Burundi.
Sylivanus Karemera anaangazia umuhimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano katika kukuza kilimo barani Afrika na uwezekano wa kulifanya bara hilo kuwa na chakula cha kutosha.
Kusikiliza makala hii, bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
habari na Dw.De

Kategori

Kategori