Showing posts with label MBEYA CITY FC. Show all posts
Showing posts with label MBEYA CITY FC. Show all posts

MBEYA CITY NA AZAM FC ZAENDELEA KUIFUKUZIA YANGA KILELENI BAADA YA KUSHINDA MICHEZO YAO LEO

TIMU ya Azam FC na Mbeya City zimeendelea kuifukuzia Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya zote kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Azam iliifunga Mtibwa Sugar uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, huku Mbeya City ikiichapa Kagare Sugar mjini Bukoba.
Ushindi huo umezifanya Azam na Mbeya City zote kufikisha pointi 30, moja nyuma ya Yanga yenye pointi 31 baada ya kushuka dimbani mara 14.
Katika mchezo wa Azam na Mtibwa, timu zote zilianza kwa kushambuliana kwa zamu, huku Azam ikionekana kulisakama lango la Mtibwa kwa kasi zaidi, lakini uimara wa mabeki wake waliweza kukoa hatari kadhaa.
Pasi iliyopigwa na Joseph Kimwaga iliweza kumpata vizuri, Tchetche aliyefunga bao hilo pekee baada ya kuweza kuwachomoka mabeki wa Mtibwa na kufumua shuti lililojaa moja kwa moja wavuni.

Kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ali, Malika Ndeule, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Brian Umony/Ismael Kone dk13/Khamis Mcha dk71, Kipre Tchetche na Joseph Kimwaga/Seif Karihe dk69.

Mtibwa Sugar; Hussein Sharrif, Hassan Ramadhani, Said Mkopi, Salim Mbonde, Salvatory Ntebe, Shaaban Nditi, Shaaban Kisiga, Masoud Ally/Abdallah Juma dk62, Juma Luizio/Mussa Mgosi dk84, Jamal Mnyate na Vincent Barnabas/Mohamed Salum dk75.

Katika mchezo mwingine, Coastal Union ilitoka sare ya kufungana bao 1-1, JKT Oljoro mchezo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Na Matukio na Vijana

WANASIASA WAPIGWA MARUFUKU TIMU YA MBEYA CITY FC


WANASIASA wanaotaka kuitumia timu ya soka ya Mbeya City kujipatia umaarufu wameonywa na kutakiwa kuacha mara moja mbwembwe zao. Wanasiasa waliopewa onyo hilo ni pamoja na wabunge ambao wamekuwa wakitoa fedha zao na ahadi kedekede kwa wachezaji na mashabiki lengo lao likiwa ni kuzidi kujiongezea umaarufu na kujiimarisha kisiasa. 
Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga alitoa onyo hilo kwenye kikao cha balaza la madiwani wa halmashauri hiyo na kusisitiza kuwa timu ya Mbeya City ni ya wakazi wa jiji la Mbeya na si ya mwana siasa yeyote wala chama chochote cha siasa. Kwa kauli hiyo ni watu wengi huenda wakatafsiri kuwa meya huyo alikuwa akiwanyooshea kidole mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa na pia mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi(Sugu) ambao wamekuwa wakishiriki mara kadhaa katika matukio mbalimbali ya timu ikiwemo kutoa fedha kuwawezesha mashabiki kuambatana na timu inapokwenda kucheza ugenini. Katika kikao hicho Kapunga alisema kuendeleza mbwembwe za kisiasa kunakofanywa na wanasiasa kunaweza kuisababishia timu kupoteza mwelekeo kwa wadau kugawanyika kwenye makundi yenye milengo tofauti ya kisiasa. “Yawezekana kuna watu hawajui historia ya Mbeya City.Hii si timu ya mwanasiasa yeyote wala chama chochote cha siasa.Sisi tuliomo humu yaani madiwani na wakazi wa jiji la Mbeya ndiyo wenye timu.Timu hii haiwahusu wabunge.Kama wataingia huko waje kama madiwani lakini si kutumia nguvu ya ubunge wao huku” 
 “Kwa wabunge wenyewe tumeanza kuwaona baada ya timu kufanya vizuri.Huko nyuma hatukumuona hata mmoja.Tumehangaika wenyewe mpaka imefikia hapa leo hii anakuja mtu anasema timu yangu.
Hilo hatulitaki.kama kuna mtu ameona kwenye timu ndiyo pa kujiongezea umaarufu wa kisiasa sisi hatutaki.” 
Alisisitiza. Kwa upande wake Dk.Mwanjelwa aliyekuwepo kwenye kikao hicho alikiri kuwa kuingia kwa wanasiasa kwenye timu kunalenga kumnufaisha mtu binafsi kisiasa na kunaweza kuisababishia timu hiyo kuingia kwenye migogoro ya kisiasa. 
NA LYAMBA LYA MFIPA 

Kategori

Kategori