Showing posts with label Israel. Show all posts
Showing posts with label Israel. Show all posts

Israel:Wanajeshi wetu hawaendi ICC

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa hatakubali wanajeshi wake kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC.
Alikuwa akizungumza katika kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri tangu Palestina ilipotuma ombi la kujiunga na mahakama ya ICC ambayo wana imani itaifungulia mashtaka Israel kwa madai ya uhalifu wa kivita katika maeneo inayokalia.
Israel imesema kuwa wanajeshi wake hawatakwenda mbele ya mahakama ya IIC kujibu mashtaka
Bwana Netanyahu ameishtumu Palestina kwa kutumia njia ya mapambano.
Israel imezuia kitita cha dola millioni 125 ufadhili wa fedha za kila mwezi kwa Palestina kama kodi inayochukua kwa niaba yake kama makubaliano ya mkataba wa amani.
Hatahivyo Palestina imepinga hatua hiyo ikitaja kama adhabu dhidi yake.
Israel yasema imeidungua ndege ya kivita ya Syria

Israel yasema imeidungua ndege ya kivita ya Syria


Jeshi la Israel limesema limeiangusha ndege ya kivita ya Syria katika milima ya Golan, ikisema ilikuwa imevuka mpaka wa usitishaji mapigano katika eneo linalokaliwa na Israel.  Hili ni tukio kubwa zaidi kutokea katika eneo hilo tangu kuanza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria mwaka wa 2011.
Image result for Israel Pix 

Taarifa iliotolewa na jeshi la Israel ambayo haikuwa na maelezo zaidi ilisema ndege hiyo iliyoingia eneo la Israel ilifanikiwa kudunguliwa muda mchache kwa mfumo wa kujilinda wa angani karibu na mpaka wa Syria. Kudunguliwa kwa ndege hiyo kunakuja wiki tatu baada ya Israel kuiangusha ndege nyengine isokuwa na rubani iliokuwa katika anga ya milima ya Golan wakati mapigano yakipamba moto upande wa Syria, ambapo eneo kubwa linashikiliwa na waasi wanaopigana kuuangusha utawala wa Bashar Al Assad. Syria imethibitisha kuangushwa kwa ndege yake ya kivita na kukielezea kitendo hicho kuwa cha uchokozi.

HIVI NDIVYO WAZIRI WA ZAMANI WA ISRAEL "ARIEL SHARON" ALIVYOZIKWA LEO




Ibaada maalum ya aliyekuwa waziri mkuu nchini Israel Ariel Sharon imefanyika nje ya majengo ya bunge la Israel.
Bwana Sharon atakumbukwa kwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa taifa la Israel lakini pia alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa jasiri aliyechukiwa na wapalestina wengi.








Waliohutubia umati,wamemtaja Sharon kama mtu aliyejitolea kuhakikisha kuna usalama kwa watu wake.
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu alisema kuwa Sharon alikuwa mmoja wa makamanda wakuu wa wayahudi na ambaye atakumbukwa zaidi ya wote.
Licha ya sifa hizo Bwana Sharon anachukiwa sana na waarabu hasa wapalestina kwa dhuluma alizowatendea chini ya utawala wake.


Kiongozi huyo aliaga dunia siku ya Jumamaosi akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa hali mahututi kwa takriban miaka minane.
Atazikwa baadaye leo katika shamba la familia yake jangwani Negev.
Maelfu ya waombolezaji walitoa heshima zao za mwisho kwa Sharon siku ya Jumapili wakati ambapo mwili wake ulikuwa umelazwa nje ya majengo ya bunge mjini Jerusalem.
Na TheChoice
Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon afariki Dunia.

Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon afariki Dunia.



Picha ya waziri mkuu wa zamani Ariel SharonPicha ya waziri mkuu wa zamani Ariel Sharo
Waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon, amefariki dunia Jumamosi akiwa na umri wa miaka 85.

Alikuwa waziri mkuu wa Israel mwaka 2001.Amekuwa mahututi tangu mwaka 2006 kufuatia mfululizo wa matatizo ya kiharusi. Ariel Sharon alikuwa askari wa vita na baadae kuwa kiongozi wa nchi.

Alipokuwa mwanajeshi, alijulikana kwa ushujaa wake katika uwanja wa mapambano kwa miongo kadhaa kufuatia kuundwa kwa taifa la Israel, akijulikana hasa wakati wa vita vya jom kippur vya mwaka 1973. Katika mbinu za hali ya juu alizozionyesha, aliwaongoza wanajeshi wa Israel kuvuka mfereji wa suez, na kulikabili jeshi la misri.

Pia alijulikana na wengi kwa kuwa jabari na mbabe. Mwaka 1982, aliongoza uvamizi wa Lebanon ambao ulipelekea mauaji yaliyofanywa na wanamgambo wa Lebanon kwa mamia ya wapalestina katika kambi za wakimbizi za sabra na shatilla huko Beirut.

Kama mwanasiasa, Ariel Sharon pia alikuwa na utatanishi. Akiwa waziri, alihamasisha kuundwa kwa makazi ya walowezi wa kiyahudi kote katika maeneo ya wapalestina.

Serikali yake ilizikandamiza vurugu katika muda wa miaka michache, na kuanza kazi ya kuweka vizuizi vya usalama ambavyo hivi sasa vinawatenga waisraeli na wapalestina.

Mwaka 2006, bwana Sharon alipata mfululizo wa matatizo ya kiharusi na kuingia katika hali ya kupoteza fahamu. Nafasi yake ya waziri mkuu ilichukuliwa na Ehud Olmert.
na Voaswahili
 Hali ya Ariel Sharon imeendelea kuwa mbaya hospitalini

Hali ya Ariel Sharon imeendelea kuwa mbaya hospitalini

Madaktari na familia ya waziri mkuu wa zamani wa Israel Ariel Sharon wanashauriana namna ya kuendelea na matibabu ya mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 85.
Sharon amepoteza fahamu kwa miaka minane, na hali yake imeendelea kuwa mbaya katika siku za karibuni.
Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa anaugua maradhi ya figo na madaktari wamesema wanahofia maisha yake. 
Sharon aipatwa na ugonjwa wa kiharusi na kuvuja damu kwenye ubongo mnamo Januari 4 mwaka wa 2006, wakati akiendelea na kampeni za uchaguzi ambao alitarajiwa kushinda. 
Alikuwa Waziri Mkuu wa Israel kuanzia mwaka wa 2001 hadi mwaka wa 2006. 
Aliunga mkono ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi katika maeneo ya wapalestina yanayokaliwa na Israel.
Israel yakosowa makubaliano ya Geneva

Israel yakosowa makubaliano ya Geneva

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameyataja makubaliano hayo kuwa ni "kosa la kihistoria." na Kuongeza kwamba kamwe hayatobadilisha nia ya Iran ya kutaka kumiliki bomu la Nyuklia
Waziri mkuu Benjamin Netanjahu na aliyekuwa waziri wa ulinzi Schaul Mofas Waziri mkuu Benjamin Netanjahu na aliyekuwa waziri wa ulinzi Schaul Mofas
Rais wa Iran Hassan Rouhani ameyataja makubaliano ya nyuklia kati ya nchi yake na nchi zenye nguvu duniani kwamba yanatambuwa haki ya nchi yake kuwa na mpango wa atomiki kwa kuridhia nchi hiyo iendelee na shughuli zake za urutubishaji wa madini ya Urani kama ilivyokuwa huko nyuma.
Katika taarifa aliyoitowa leo (24.11.2013) kupitia kituo cha televisheni ya taifa, Rouhani amesema mazungumzo yatafanyika mara moja juu ya makubaliano kamili ya pande mbili, na kwamba nchi yake ina nia ya dhati ya kuyazingatia mara moja makubaliano hayo.
Aliweka wazi pia kwamba mafanikio ya mazungumzo ya nyuklia yametokana na muongozo uliotolewa na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.
Mawaziri wa nje,William Hague,Mohammad Javd Zarif,Guido Westerwelle na mkuu wa sera za nje wa EU Catherine Ashton Mawaziri wa nje,William Hague,Mohammad Javd Zarif,Guido Westerwelle na mkuu wa sera za nje wa EU Catherine Ashton
Kilichomo kwenye makubaliano
Makubaliano hayo ya mwanzo yaliyofikiwa mjini Geneva yamepongezwa na Urusi. Waziri wake wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov amesema ni hatua itakayozifaidisha pande zote.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo Iran imekubali kuzuia mpango wake wa nyuklia angalau kwa miezi sita, wakati nchi zenye nguvu zikiahidi kuiondolea vikwazo kadhaa.
Aidha Iran imekubali kutowa nafasi kwa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nishati ya Nyuklia (IAEA) kufanya ukaguzi mpana katika mitambo yake ya nyuklia, kitendo ambacho bila ya shaka kimeongeza hali ya kuaminiana iliyohitajika katika eneo la Ghuba na Mashariki ya Kati na kupunguza hofu juu ya mpango huo wa Iran
Msimamo wa Israel na Marekani
Hata hivyo, Israel haikupendezwa na hatua ya nchi zenye nguvu, huku Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akiyataja makubaliano kuwa ni "kosa la kihistoria." Netanyahu ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Tel-Aviv kwamba awamu hiyo ya mwanzo ya makubaliano haitoifanya Iran kusimamisha kile ilichokiita nia ya kutengeneza silaha za nyuklia, lakini akaapa "kutokuiruhusu Iran" kuwa na silaha hizo.
Pamoja na kauli hiyo ya waziri mkuu, upande wa maafisa wa kijeshi na serikali ya Israel umekiri kwamba kulikuwa hakuna la kufanyika kuzuia makubaliano hayo mjini Geneva.
Israel lakini imesema itafanya kila iwezalo kuwa na ushawishi katika makubaliano ya mwisho ambayo yatajadiliwa katika kipindi cha miezi sita. Kimsingi taifa hilo la Kiyahudi lina amini kwamba Iran inajaribu kutengeneza bomu la nyuklia na katika kipindi cha wiki kadhaa kabla ya makubaliano ya Jumapili lilionya kwamba makubaliano yatakayofikiwa hayatoshelezi.
Rais Barack Obama wa Marekani Rais Barack Obama wa Marekani
Waziri wa Israel anayehusika na masuala ya ujasusi na ambaye miongoni mwa majukumu yake ni kufuatilia mpango wa nyuklia wa Iran, Yuval Steinitz, amesema makubaliano ya nchi zenye nguvu na Iran bado ni mabaya na yataifanya hali kuwa ngumu zaidi kuliko ilivyokuwa katika kupatikana suluhisho linalohitajika hapo baadaye.
Steinitz amesema ni hatua itakayoiweka Iran karibu na umiliki wa bomu huku akiifananisha hatua ya makubaliano hayo kuwa kama ile ya mwaka 2007 kati ya jumuiya ya kimataifa na Korea ya Kaskazini iliyoshindwa.
Mshirika wa karibu wa Israel, Marekani imeyaridhia matokeo ya mkutano wa Geneva ambapo taarifa iliyotoka Ikulu ya White House imeyataja makubaliano hayo ya nyuklia kama hatua ya mwanzo katika mazungumzo ya miezi sita. Rais Barack Obama amesema sasa Iran inapaswa kuonesha ukweli wa dhamira yake ya nyuklia kwa matumizi ya amani.
Rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy (kushoto) na mkuu wa Tume ya Umoja huo Jose Manuel Barrosso Rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy (kushoto) na mkuu wa Tume ya Umoja huo Jose Manuel Barrosso
Lakini taarifa hiyo pia imebainisha kwamba vikwazo katika masuala muhimu kama mafuta, benki na fedha vitabakia na kusisitiza ikiwa Iran itakwenda kinyume na makubaliano yaliyofikiwa basi hatua ya nchi hiyo kupunguziwa vikwazo itabatilishwa.
Kinachosemwa na Umoja wa Ulaya
Rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy amepongeza ujasiri ulioonyeshwa na Iran na nchi zenye nguvu Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, China na Urusi. Van Rompuy amesema ni muhimu hivi sasa kuhakikisha utekelezaji unazingatiwa kama inavyohitajika kwa mujibu wa makubaliano.
Mkuu huyo wa Umoja wa Ulaya ameelezea matumani yake kwamba kushughulikia kwa suala hili kutaleta mabadiliko makubwa katika eneo zima na duniani kwa ujumla, ambayo ameyataja ni kupunguwa kwa misuguano ya kisiasa pamoja na kuchangia kuleta hali ya kuaminiana na uungaji mkono wa hatua za kupunguza utapakazaji wa silaha za maangamizi makubwa.
Na DW.DE 

Kategori

Kategori