Taarifa kutoka TASABA, UONGOZI WA TASABA. Kupitia rais Prosper Mwakitwange. Unatangaza ya kuwa kulingana, na taarifa za msiba,ni kwamba tupo katika legal process za kukabithiwa mwili wa ndugu yetu, ambapo tunataraji kufanikisha Leo. Na baadae tutatangaza process zinazofuatia nikifanikiwa, na balozi ambaye kwa sasa yupo Bangalore, nitawatangazia hatua tuliofikia na muwajulisha wapi na mahali tutakutana, naomba mjitaarishe tukiwajulisha mfike bila ya kukosa. Mungu ibariki TASABA, MUNGU Ibariki Tanzania.
: TAARIFA ZA MSIBA, UONGOZI WA TASABA. Unasikitika kutangaza MSIBA wa Mwanachama na Mwanafunzi mwezetu, CHRISTIAN BENJAMIN MUTANDIS, alikuwa anasoma Koshys College, second year, BCA course. Kilichotokea jioni ya Leo, kwa ajali ya pikipiki. Taratibu za kuuwaga mwili,ibada na misa na sala fupi tutatangaza kesho Taratibu zote na mahali tutapokutana pamoja na kuuwaga mwili. Tunawaomba tushirikiane kwenye kipindi hichi kigumu na familia yake. Bwana ametoa na Bwana ametwa, Jina lake lihimidiwe.
Kutokea kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa kwa usawa kwa duniani kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi kutokana na maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki.
Takriban watoto 8 kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu hii kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa takwimu sahihi katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD barani Afrika inaweza kuwa wengi sana.
Watoto wenye ugonjwa wa moyo wanaweza kuonesha dalili wakati wa kuzaliwa. baadhi ya dalili hizi ni pamoja mtoto kubadilika rangi na kuwa wa bluu, mtoto kupumua kwa kasi, jasho nyingi, kuvurugika kwa mapigo ya moyo, kushindwa kula ambapo husababisha kushindwa kuongezeka uzito na mtoto kupata maambukizi katika mfumo wa upumuaji mara kwa mara.
Wakati mwingine, hii inaweza kugundulika kwa kuhakikisha unamuona daktari wa watoto wachanga mara kwa mara. Tatizo lolote katika moyo linaweza kubadilisha namna moyo unavyosikika. Sauti hizi zisizo za kawaida zinaweza kugunduliwa na daktari kwa kusikiliza kutumia kifaa maalumu cha ‘stethoskopu’. Kuna baadhi ya matukio ambapo vichanga na watoto wadogo wanakuwa wakizimia, kuonyesha kwamba wako katika hali ya kushindwa kwa mizunguko upumuaji.
Watoto, hasa walio chini ya umri wa siku 28 na vichanga ambao wako chini ya umri wa mwaka mmoja hawachukuliwi kama vijana, hivyo kuwafanyia upasuaji moyo kwao ni changamoto. Inapaswa kuzingatiwa kuwa moyo wa mtoto anapozaliwa unakuwa na ukubwa wa ngumi yake. Kutokana na muundo wake unaochanganya, watoto wachanga hukabiliwa na kiwango kidogo cha ufanyaji kazi wa moyo na hivyo kupata uharibifu kwa viungo vingine muhimu ikiwa ni pamoja na mapafu, figo na ini. Hivyo, kwa asili upasuaji wa moyo ni mgumu zaidi.
Kutokana na ugumu wa upasuaji kwa mtoto, Dkt. Neville A.G Solomon Mshauri, Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai anaona kwamba mbinu zinazojumuisha mambo mbalimbali zitumike ili kuwa na mafanikio. Ili kufanya kwa usahihi upasuaji na marekebisho bila kuharibu miundo yoyote muhimu, mpasuaji ni muhimu kuusimamisha moyo wa mtoto, kukata usambazaji wa damu kwenye moyo na kukausha damu yote ili aweze kuona vema miundo ya ndani. Pamoja na utaratibu huu mgumu, wakati wa upasuaji ni wa muhimu na makini sana. Ugumu huongezeka kadiri upasuaji unapochukua muda mrefu. Ni muhimu kwa timu nzima kufanya kazi katika hali ya maelewano kwa lengo la pamoja la kuokoa maisha.
Wakati mtoto anapohisiwa kuwa na ugonjwa wa moyo hatua ya awali ya kuchunguza hili ni kwa kufanya vipimo kama vile kuchukua X-ray ya kifua na ECG ambapo husaidia kuthibitisha uchunguzi. Mionzi ya sauti ya moyo (ECG) mara nyingi husaidia katika uchunguzi. Hii itatoa taarifa za kutosha kwa ajili ya mtaalamu na / au mpasuaji wa moyo na kuamua namna matibabu yanavyopaswa kufanyika. Kama vipimo vya ziada au zaidi vinahitajika, takwimu hizi zinaweza kupatikana kwa njia za uchunguzi kama wa kutumia katheta ya moyo na ‘anjiografia’, CT na MRI ‘anjiogramu’ ya moyo.
Uboreshaji wa hatua hizi za uchunguzi umeongezeka ubora wa upasuaji kwa watoto. Daktari mpasuaji au mtaalamu wa moyo sasa utakuwa na mwongozo wa pande tatu za ugonjwa wa moyo kabla ya utekelezaji wa wake. Hii inatoa mpango bora wa upasuaji usiokabiliwa na matatizo wakati wa upasuaji na kwa hiyo matokeo ya upasuaji kuwa bora zaidi na yenye mafanikio zaidi.
Kuna tiba kadhaa ambazo zinapatikana kwa sasa. Baadhi ya hizi ni pamoja na mbinu ya kutumia matundu madogo na upasuaji wa moyo kwa kuufungua na kuufunga. Mbinu ya matundu huweza kukamilika kwa siku moja tu na hii inaweza kufanywa na wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu wa magonjwa ya moyo kwa watoto. Utaratibu huu unahitaji kupatikana kwa vifaa vinavyowezesha kuipata mashimo midogo ya moyo ambayo imefungwa na valvu na kujificha ndani sana. Kwa mbinu hii mtoto hapati maumivu ya kukatwa. Utaratibu huu hauhitaji mashine ya upumuaji kuwekwa au mtoto kuwekwa katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi mtoto anaweza kupona kwa haraka zaidi na kurudi shule na hata kushiriki katika michezo.
Namna nyingine za matibabu ambazo zinaweza kutumika kwa watoto wenye hali mbaya zaidi ya moyo ni ile ya kuufungua na kuufunga moyo yaani (upasuaji). Upasuaji huu unaweza kufanywa kwa watoto wachanga wenye umri wa masaa manne hadi matano au wenye gramu 800. Kutokana na utata wa hali hii, umuhimu wa kutumia timu shirikishi unasisitizwa zaidi. Hata mtaalamu wa upasuaji awe mjuzi sana, atahitaji msaada kutoka kwa timu.
Watu kadhaa wanahusika katika mchakato huu. Wauguzi wanashiriki katika kuwahudumia watoto ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo. Madaktari wa watoto wanashiriki kuwahuduma baada ya upasuaji kama vile kudhibiti maumivu, kudhibiti maambukizi na msaada wa kisaikolojia na teknolojia ya kisasa inaruhusu usahihi zaidi katika uchunguzi. Hii ni sehemu muhimu zaidi kuhakikisha maisha ya mtoto yanaendelea.
Kwa mujibu wa Dkt Neville A.G Solomon wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai, kinga ni bora kuliko tiba. Kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza kujaribu na kuzuia ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa. Kliniki (ya mjamzito) kupata kipimo maalumu kitaalamu ‘echocardiography, ambacho hutumika kuchunguza moyo wa mtoto akiwa ndani tumbo la mama.
Daktari bingwa wa Moyo unaweza kutambua kasoro za moyo mapema wiki ya kumi na nane ya ujauzito. Kwa hiyo ‘echocardiogram’ itawezesha wazazi kufanya maamuzi sahihi juu ya mustakabali wa mtoto kama kuna kasoro zilizogundulika katika moyo.
Njia nyingine ambayo inaweza kuzuia au kupunguza hatari kwa kuepukana ndoa kati ya ndugu wa damu, kwa mama kuacha kutumia baadhi ya madawa, na kuepuka mionzi wakati wa ujauzito huweza kumfanya mtoto kuzaliwa na kasoro katika moyo na pia mama kuepuka maambukizi. Njia ya kawaida ya kuepuka ugonjwa wa baridi yabisi katika moyo wa mtoto ni kwa kupatiwa matibabu ya maambukizi katika koo kwa wakati kwa kutumia antibiotiki.
Timu ya wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto Hospitali ya Apollo Chennai inaona fahari kubwa kupambana dhidi ya maradhi ya moyo kwa watoto duniani kote. Hii imewezekana kutokana na uvumbuzi mashine za mawimbi ya sauti zinazobebeka na za ukubwa wa kompyuta ndogo (mpakato). Hii Inawawezesha kufika sehemu za mbali zaidi duniani na kuchunguza kasoro na magonjwa ya moyo.
Baada ya upasuaji ingawa watoto wengi hutibiwa kikamilifu bado watahitaji ufuatiliaji kwa miaka ijayo. Baadhi wanaweza kuhitaji kurudiwa upasuaji hata hivyo wengi hawatahitaji dawa tena na kuwa na uwezo wa kuendelea na maisha ya kawaida kama watoto wengine. Wataweza wa kuishi wakiwa afya kwa muda mrefu maishani bila matatizo.
Inachangiwa na:
Dk Neville A.G Solomon
Mshauri, Mtaalamu Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto
Mtoto wa ajabu aliyezaliwa March 26 mwaka huu ambaye anasemaka kuwa mtoto wa ajabu kuliko watoto wote waliozaliwa kwa mwaka huu ambaye anasura kama tembo aliyezaliwa India anayetukuzwa kama mungu nchini kwao.Katika kijiji alichozaliwa mtoto huyo cha Aligarh, Uttar Pradesh India. Kwa mujibu wa Daktari alisema hali ya mtoto huyo inasababishwa na urithi kutoka kwa mama na baba yake (genetic mutation). Kwa mujibu wa shangazi wa mtoto huyo anasema "My sister-in-law gave birth to a girl and her face looks exactly like Lord Ganesha. Everybody is saying she is an incarnation of the god. This is why whoever hears about her is coming here to get a glimpse of the baby and are making whatever offerings possible."Anafanana na mungu wa Ganesha.
Balozi wa India nchini Tanzania anayemaliza muda wake wa kazi, Mhe.Debnath Shaw akitoa hotuba yake ya kuaga mbele ya wageni waalikwa wakiwemo baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Julai, 2015.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto) pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini ambaye pia ni mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe.Juma Halfan Mpango wakifuatilia hotuba ya Mhe.Debnath Shaw (hayupo pichani).
Balozi wa China hapa nchini, Mhe.LU Youqing (kulia) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi.Eliet Magogo (katikati) pamoja na mmoja wa wageni waalikwa wakisikiliza hotuba.
Mabalozi pamoja na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifurahia hotuba ya Balozi huyo wa India hapa nchini.
Balozi Yahya kwa pamoja na Balozi Shaw wakitakiana afya njema
Mshereheshaji akiendelea kusherehesha wakati wa hafla hiyo.
Balozi Yahya akiwaongoza Balozi Shaw (kulia) na Balozi Mpango kupata chakula wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchan akumuaga Balozi Shaw.
Balozi Yahya akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Shaw na Balozi Mpango
Picha ya Pamoja.
Balozi Simba akibadilishana mawazo na Balozi Debnath Shaw mara baada ya hafla hiyo.
Balozi Simba akiagana na Balozi Juma Mpango baada ya hafla hiyoPicha na Reuben Mchome
"Sitamwaacha binti yangu ateseke kama mimi ninavyoteseka nikiwa katika siku zangu. Familia yangu inafanya nijihisi najisi.
"Siruhusiwi kwenda jikoni, Siwezi kuingia hekaluni, Siwezi kukaa na wengine."
Kuna hisia ya
dhamira katika sauti ya Manju Baluni mwenye umri wa miaka 32.
Nilikutana naye katika kijiji cha Uttarakhand, jimbo lenye miinuko
kaskazini mwa India.
Nchini India,kuna ukimya kuhusu suala la afya
ya wanawake, hususan wawapo katika siku zao. Kuna mwiko uliojikita
katika jamii hizi kuhusu suala la mwanamke awapo katika hedhi: wanawake
si wasafi, wachafu, wagonjwa na wakati mwingine wamelaanika katika
kipindi hicho.
'Wasiwasi na Mashaka'
Watu wanaamini kuwa wanawake wanaokuwa katika hedhi hawatakiwi kuoga na wana upungufu wa damu.
Uchunguzi wa hivi karibuni wa kampuni ya kutengeneza taulo maalum za kujisitiri kina mama
wanapokuwa katika hedhi umeonyesha kuwa asilimia 75% ya wanawake
wanaoishi mijini bado wananua taulo hizo zikiwa zimefungwa katika mifuko
au gazeti ili kutoonyesha kilichomo ndani kwa sababu ya aibu
inayohusishwa na hedhi.
Mwanamke akikunja taulo za kujihifadhi wakati wa siku zake nchini India
Na kamwe hawawaombi wanaume katika familia kuwanunulia taulo hizo maalum.
Nimekulia katika nyumba yenye wanawake wengi, lakini bado hatuwezi kujadili kwa uwazi suala hili ambalo ni la kawaida.
Wasichana
wanajifunza kuficha nguo zao wanazotumia wawapo kwenye hedhi kwa
wanaume baada ya kuzifua, anasema Rupa Jha. Mama yangu alitumia mashuka
makuu kuu na kuzificha katika sanduku, tayari kwa kutumiwa na mabinti
zake wanne.
Changamoto
kubwa ni namna ya kukausha vipande hivyo vya nguo. Nina kumbukumbu za
kuhisi wasiwasi na mashaka juu ya mchakato mzima.
Nilifundishwa mbinu nadada
zangu wakubwa - namna ya kuficha nguo zenye madoa ya damu chini ya nguo
nyingine bila ya mwanaume yeyote kugundua. Hatukuthubutu kuziacha peupe
kwenye jua ili zikauke kabisa.
Nilihisi 'mchafu sana'
Matokeo ni kwamba kamwe hazikukauka vizuri, ziliacha harufu ya uvundo. Nguo hizo zisizo safi zilitumika tena na tena.
Wanawake wakisikiliza mwezeshaji kuhusu hali zao za usafi nchini India
Ukosefu wa maji ulifanya kazi
ya ufuaji kuwa ngumu na isiyo na usafi. Hali hiyo haijabadilika sana
tangu wakati huo kwa wanawake wengi wa Kihindi.
Uchunguzi mwingi
uliofanyika siku za karibuni umeonyesha kuwa mila hizi zimesababisha
madhara makubwa ya kiafya. Imeripotiwa kuwa mmoja kati ya wasichana
watano nchini India anaacha masomo kutokana na kadhia ya hedhi.
Baadhi
ya wasichana wanaacha kwenda shule wawapo katika kipindi cha hedhi.
Margdarshi mwenye umri wa miaka kumi na mitano anaishi katika kijiji cha
ndani cha Uttarakashi.
Anapenda kwenda shule japo inamaanisha safari
ngumu akipita katika eneo lenye vilima vikali. Kamwe hajawahi kukosa
masomo, isipokuwa kwa mwaka jana wakati ambapo nusura aache masomo baada
ya kupata siku zake kwa mara ya kwanza.
"Tatizo kubwa kuliko yote
ilikuwa namna ya kukabiliana na hali hiyo. Bado lipo. Najisikia
kufedheheshwa, hasira na mchafu sana. Mwanzoni niliacha kwenda shule."
'Suala la kibinadamu'
Anataka kuwa daktari na anashangaa kwa nini wavulana katika darasa lake wakati wa somo la elimu ya viumbe(baolojia) wanacheka sana mwalimu anapoelezea njia ya hedhi.
"Nachukia.
Natamani tungekuwa huru zaidi na kujisikia huru tunapozungumzia suala
hili. Hali hii inatokea kwa kila mwanamke kwa hiyo kuna nini cha
kuchekesha hapo?"
Mama nchini India
Anshu Gupta, mwanzilishi wa
shirika lisilo la kiserikali, Goonj, anahisi kuwa tatizo hili limejikita
katika ukweli kwamba linahusishwa na wanawake.
Nchini India
wanawake wanatumia taulo za kujihifadhi wakati wawapo katika siku zao
kwa kutumia nguo kuu kuu. "Si suala la wanawake pekee. Ni suala la
kibinadamu lakini tumelibagua. Baadhi yetu tunataka kuondokana na
utamaduni huu wa kuona aibu na kunyamaza. Tunahitaji kuvunja utamaduni
huu."
Shirika hili linafanya kazi katika majimbo 21 kati ya 30.
Shirika
hili pia linatengeneza taulo rahisi kutokana na nguo zilizochakatwa
upya ili kuwasaidia asilimia 70% ya wanawake wa India ambao hawawezi
kupata taulo salama na safi.
Muhimu zaidi, wanaanza kuzungumzia suala hili. Bila kuhisi kufedheheka.
Makala ya BBC ya BBC's 100 Women yamekuwa yakitangazwa katika mtandao, katika televisheni na radio
ya Idhaa ya Dunia tangu Oktoba 27-29. Changia maoni yako katika
mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, ukitumia alama #100Women.
Rais wa Uchina, Xi Jingping, amewasili nchini India na kutoa mwito wa ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili kwa manufaa ya maendeleo. Rais Xi Jinping, amesema kuwa nchi zote mbili ziko katika hatua muhimu za mabadiliko na maendeleo. Amesifia faida za muungano na ushirikiano wa mataifa hayo mawili. Ziara hiyo inatazamia kuboresha uhusiano kati ya mataifa huyo mawili ambayo kwa muda mrefu ulikuwa mmbovu. Mwenyeji wake atakuwa Waziri Mkuu mpya wa India, Narendra Modi, ambaye amewahi kutangaza wazi kuwa anapendelea uongozi wa uchina na kuwa anatafuta njia ya kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo. Wanatarajiwa kutia sahihi ushirikiano wa kibiashara wa mabillioni ya madola katika uwekezaji wa China katika harakati za kuimarisha uhusiano na Waziri Mkuu mpya wa India, Narendra Modi, licha ya mvutano wa msingi kuhusu mpaka wao na ushindani wao wa ushawishi wa kikanda. Rais Xi amekutana na waziri mkuu wa Narendra Modi wa India Mataifa hayo mawili ambayo yanazozania mpaka yanangangania umashuhuri katika eneo lao na rasilmali za nishati. Swala lingine linalotatanisha kati yao ni kuwa kiongozi wa Tibet aliye uhamishoni, Dalai Lama, anaishi Kaskazini mwa India. Ameombwa aahirishe ziara yake ya New Delhi ili isigongane na ile ya Bwana Xi. Lakini shughuli za kibiashara kati ya mataifa hayo zinaimarika kwa kuwa inatarajiwa kwamba Bwana Xi ataleta nchini India uekezaji wa zaidi ya Dola Bilioni 100.