Showing posts with label India. Show all posts
Showing posts with label India. Show all posts

MTANZANIA MWANAFUNZI MWINGINE AFARIKI INDIA LEO HII ..KIFO CHAKE CHAZUA UTATA BARABARANI








Taarifa kutoka TASABA, 
UONGOZI WA TASABA. Kupitia rais Prosper Mwakitwange.
Unatangaza ya kuwa kulingana, na taarifa za msiba,ni kwamba tupo katika legal process za kukabithiwa mwili wa ndugu yetu, ambapo tunataraji kufanikisha Leo. Na baadae tutatangaza process zinazofuatia nikifanikiwa, na balozi ambaye kwa sasa yupo Bangalore, nitawatangazia hatua tuliofikia na muwajulisha wapi na mahali tutakutana, naomba mjitaarishe tukiwajulisha mfike bila ya kukosa. 
Mungu ibariki TASABA,
MUNGU Ibariki Tanzania.


: TAARIFA ZA MSIBA, 
UONGOZI WA TASABA.
Unasikitika kutangaza MSIBA wa Mwanachama na Mwanafunzi mwezetu, CHRISTIAN BENJAMIN MUTANDIS, alikuwa anasoma Koshys College, second year, BCA course. Kilichotokea jioni ya Leo, kwa ajali ya pikipiki.
Taratibu za kuuwaga mwili,ibada na misa na sala fupi tutatangaza kesho Taratibu zote na mahali tutapokutana pamoja na kuuwaga mwili.
Tunawaomba tushirikiane kwenye kipindi hichi kigumu na familia yake. 
Bwana ametoa na Bwana ametwa, 
Jina lake lihimidiwe.

MADAKTARI BINGWA WA MOYO TOKA INDIA, WANATARIJIWA KUPAMBANA NA UGONJWA WA MOYO WA KUZALIWA KWA WATOTO




Na Mwandishi Wetu ,
Kutokea kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa kwa usawa kwa duniani kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi kutokana na maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki.

 Takriban watoto 8 kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu hii kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa takwimu sahihi katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD barani Afrika inaweza kuwa wengi sana.

Watoto wenye ugonjwa wa moyo wanaweza kuonesha dalili wakati wa kuzaliwa. baadhi ya dalili hizi ni pamoja mtoto kubadilika rangi na kuwa wa bluu, mtoto kupumua kwa kasi, jasho nyingi, kuvurugika kwa mapigo ya moyo, kushindwa kula ambapo husababisha kushindwa kuongezeka uzito na mtoto kupata maambukizi katika mfumo wa upumuaji mara kwa mara. 

Wakati mwingine, hii inaweza kugundulika kwa kuhakikisha unamuona daktari wa watoto wachanga mara kwa mara. Tatizo lolote katika moyo linaweza kubadilisha namna moyo unavyosikika. Sauti hizi zisizo za kawaida zinaweza kugunduliwa na daktari kwa kusikiliza kutumia kifaa maalumu cha ‘stethoskopu’. Kuna baadhi ya matukio ambapo vichanga na watoto wadogo wanakuwa wakizimia, kuonyesha kwamba wako katika hali ya kushindwa kwa mizunguko upumuaji.

Watoto, hasa walio chini ya umri wa siku 28 na vichanga ambao wako chini ya umri wa mwaka mmoja hawachukuliwi kama vijana, hivyo kuwafanyia upasuaji moyo kwao ni changamoto. Inapaswa kuzingatiwa kuwa moyo wa mtoto anapozaliwa unakuwa na ukubwa wa ngumi yake. Kutokana na muundo wake unaochanganya, watoto wachanga hukabiliwa na kiwango kidogo cha ufanyaji kazi wa moyo na hivyo kupata uharibifu kwa viungo vingine muhimu ikiwa ni pamoja na mapafu, figo na ini. Hivyo, kwa asili upasuaji wa moyo ni mgumu zaidi.

Kutokana na ugumu wa upasuaji kwa mtoto, Dkt. Neville A.G Solomon Mshauri, Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai anaona kwamba mbinu zinazojumuisha mambo mbalimbali zitumike ili kuwa na mafanikio. Ili kufanya kwa usahihi upasuaji na marekebisho bila kuharibu miundo yoyote muhimu, mpasuaji ni muhimu kuusimamisha moyo wa mtoto, kukata usambazaji wa damu kwenye moyo na kukausha damu yote ili aweze kuona vema miundo ya ndani. Pamoja na utaratibu huu mgumu, wakati wa upasuaji ni wa muhimu na makini sana. Ugumu huongezeka kadiri upasuaji unapochukua muda mrefu. Ni muhimu kwa timu nzima kufanya kazi katika hali ya maelewano kwa lengo la pamoja la kuokoa maisha.

Wakati mtoto anapohisiwa kuwa na ugonjwa wa moyo hatua ya awali ya kuchunguza hili ni kwa kufanya vipimo kama vile kuchukua X-ray ya kifua na ECG ambapo husaidia kuthibitisha uchunguzi. Mionzi ya sauti ya moyo (ECG) mara nyingi husaidia katika uchunguzi. Hii itatoa taarifa za kutosha kwa ajili ya mtaalamu na / au mpasuaji wa moyo na kuamua namna matibabu yanavyopaswa kufanyika. Kama vipimo vya ziada au zaidi vinahitajika, takwimu hizi zinaweza kupatikana kwa njia za uchunguzi kama wa kutumia katheta ya moyo na ‘anjiografia’, CT na MRI ‘anjiogramu’ ya moyo.

Uboreshaji wa hatua hizi za uchunguzi umeongezeka ubora wa upasuaji kwa watoto. Daktari mpasuaji au mtaalamu wa moyo sasa utakuwa na mwongozo wa pande tatu za ugonjwa wa moyo kabla ya utekelezaji wa wake. Hii inatoa mpango bora wa upasuaji usiokabiliwa na matatizo wakati wa upasuaji na kwa hiyo matokeo ya upasuaji kuwa bora zaidi na yenye mafanikio zaidi.

Kuna tiba kadhaa ambazo zinapatikana kwa sasa. Baadhi ya hizi ni pamoja na mbinu ya kutumia matundu madogo na upasuaji wa moyo kwa kuufungua na kuufunga. Mbinu ya matundu huweza kukamilika kwa siku moja tu na hii inaweza kufanywa na wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu wa magonjwa ya moyo kwa watoto. Utaratibu huu unahitaji kupatikana kwa vifaa vinavyowezesha  kuipata  mashimo midogo ya moyo ambayo imefungwa na valvu na kujificha ndani sana. Kwa mbinu hii  mtoto hapati maumivu ya kukatwa. Utaratibu huu hauhitaji  mashine ya upumuaji kuwekwa au mtoto kuwekwa katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi mtoto anaweza kupona kwa haraka zaidi na kurudi shule na hata kushiriki katika michezo.

Namna  nyingine za matibabu ambazo zinaweza kutumika kwa watoto wenye hali mbaya zaidi ya moyo ni ile ya kuufungua na kuufunga moyo yaani (upasuaji). Upasuaji huu unaweza kufanywa kwa watoto wachanga wenye umri wa masaa manne hadi matano au wenye gramu 800. Kutokana na utata wa hali hii, umuhimu wa kutumia timu shirikishi unasisitizwa zaidi. Hata mtaalamu wa upasuaji awe mjuzi sana, atahitaji msaada kutoka kwa timu.

Watu kadhaa wanahusika katika mchakato huu. Wauguzi wanashiriki katika kuwahudumia watoto ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo. Madaktari wa watoto wanashiriki kuwahuduma baada ya upasuaji kama vile kudhibiti maumivu, kudhibiti maambukizi na msaada wa kisaikolojia na teknolojia ya kisasa inaruhusu usahihi zaidi katika uchunguzi. Hii ni sehemu muhimu zaidi kuhakikisha maisha ya mtoto yanaendelea.

Kwa mujibu wa Dkt Neville A.G Solomon wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai, kinga ni bora kuliko tiba. Kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza kujaribu na kuzuia ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa. Kliniki (ya mjamzito) kupata kipimo maalumu kitaalamu ‘echocardiography, ambacho hutumika kuchunguza moyo wa mtoto akiwa ndani tumbo la mama.

 Daktari bingwa wa Moyo unaweza kutambua kasoro za moyo mapema wiki ya kumi na nane ya ujauzito. Kwa hiyo ‘echocardiogram’ itawezesha wazazi kufanya maamuzi sahihi juu ya mustakabali wa mtoto kama kuna kasoro zilizogundulika katika moyo.

Njia nyingine ambayo inaweza kuzuia au kupunguza hatari kwa kuepukana ndoa kati ya ndugu wa damu, kwa mama kuacha kutumia baadhi ya madawa, na kuepuka mionzi wakati wa ujauzito huweza kumfanya mtoto kuzaliwa na kasoro katika moyo na pia mama kuepuka maambukizi. Njia ya kawaida ya kuepuka ugonjwa wa baridi yabisi katika moyo wa mtoto ni kwa kupatiwa matibabu ya maambukizi katika  koo kwa wakati kwa kutumia antibiotiki.

Timu ya wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto Hospitali ya Apollo Chennai inaona fahari kubwa kupambana dhidi ya maradhi ya moyo kwa watoto duniani kote. Hii imewezekana kutokana na uvumbuzi mashine za mawimbi ya sauti zinazobebeka na za ukubwa wa kompyuta ndogo (mpakato). Hii Inawawezesha kufika sehemu za mbali zaidi duniani na kuchunguza kasoro na magonjwa ya moyo.

Baada ya upasuaji ingawa watoto wengi hutibiwa kikamilifu bado watahitaji ufuatiliaji kwa miaka ijayo. Baadhi wanaweza kuhitaji kurudiwa upasuaji hata hivyo wengi hawatahitaji dawa tena na kuwa na uwezo wa kuendelea na maisha ya kawaida kama watoto wengine. Wataweza wa kuishi wakiwa afya kwa muda mrefu maishani bila matatizo.

Inachangiwa na:
Dk Neville A.G Solomon
Mshauri, Mtaalamu Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto
Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai.

MAAJABU: KUMBE YULE MTOTO WA AJABU ALIYEZALIWA INDIA ANAFANANA NA MUNGU WAO



Mtoto wa ajabu aliyezaliwa March 26 mwaka huu ambaye anasemaka kuwa mtoto wa ajabu kuliko watoto wote waliozaliwa kwa mwaka huu ambaye anasura kama tembo aliyezaliwa India anayetukuzwa kama mungu nchini kwao.Katika kijiji alichozaliwa mtoto huyo cha Aligarh, Uttar Pradesh India.


Kwa mujibu wa Daktari alisema hali ya mtoto huyo inasababishwa na urithi kutoka kwa mama na baba yake (genetic mutation). Kwa mujibu wa shangazi wa mtoto huyo anasema
"My sister-in-law gave birth to a girl and her face looks exactly like Lord Ganesha. Everybody is saying she is an incarnation of the god. This is why whoever hears about her is coming here to get a glimpse of the baby and are making whatever offerings possible."Anafanana na mungu wa Ganesha.

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAMUAGA BALOZI WA INDIA ALIYEMALIZA MUDA WA KAZI NCHINI


Balozi wa India nchini Tanzania anayemaliza muda wake wa kazi, Mhe.Debnath Shaw akitoa hotuba yake ya kuaga mbele ya wageni waalikwa wakiwemo  baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Julai, 2015.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto) pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini ambaye pia ni mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe.Juma Halfan Mpango wakifuatilia hotuba ya Mhe.Debnath Shaw (hayupo pichani).
Balozi wa China hapa nchini, Mhe.LU Youqing (kulia) pamoja na Afisa  Mambo ya Nje, Bi.Eliet Magogo (katikati) pamoja na mmoja wa wageni waalikwa wakisikiliza hotuba.

Mabalozi pamoja na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifurahia hotuba ya Balozi huyo wa India hapa nchini.
Balozi Yahya kwa pamoja na  Balozi Shaw wakitakiana afya njema
 Mshereheshaji akiendelea kusherehesha wakati wa hafla hiyo.
Balozi Yahya akiwaongoza Balozi  Shaw (kulia) na Balozi  Mpango kupata chakula wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchan akumuaga Balozi Shaw.
 Balozi Yahya akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Shaw na Balozi Mpango
 Picha ya Pamoja.
 Balozi Simba akibadilishana mawazo na Balozi Debnath Shaw mara baada ya hafla hiyo.
Balozi Simba akiagana na Balozi Juma Mpango baada ya hafla hiyo Picha na Reuben Mchome

Kategori

Kategori