Showing posts with label 2017 at 12:13PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 12:13PM. Show all posts
Maalim Seif Apata Pigo Kubwa zaidi Kutoka Kwa Lipumba, Bodi ya Lipumba Yasajiliwa na Ruzuku itakuwa yao

Maalim Seif Apata Pigo Kubwa zaidi Kutoka Kwa Lipumba, Bodi ya Lipumba Yasajiliwa na Ruzuku itakuwa yao

Kambi ya Cuf ya Ibrahim Lipumba imethibitisha bodi yao kupata usajili mpya kutoka RITA na sasa bodi ya wadhamini ya zamani imefutwa
Kwa sasa miamala yote ikiwemo ruzuku itakuwa inaingia kwenye akaunti na watakuwa wanachukua upande wa Lipumba na kutokana na bodi hiyo kufutwa wamesema kesi zilizokuwa zimefunguliwa dhidi yao na bodiya zamani watahakikisha zimefutwa.
Upande wa maalim seif wamesema kwa sasa hawana cha kuzungumza hadi watakapokaa
RITA walipopigiwa simu hawakupokea.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2stlx9X
via IFTTT


Cristiano Ronaldo apata watoto mapacha.

Cristiano Ronaldo apata watoto mapacha.

Miezi iliyopita tuliandika juu ya tetesi za kuwepo kwa mwanamke mmoja ambaye hajulikani ni nani lakini alikuwa na mimba ya mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo, jambo hilo limekuwa siri kubwa katika familia ya Ronaldo lakini hadi mama yake mzazi analijua hilo.
Sasa taarifa mpya zinasema siku ya Alhamisi mwanamke huyo amejifungua watoto mapacha wa kike na wa kiume ambao wanafahamika kwa majina ya Mateo na Eva, kituo kimoja cha habari nchini Ureno kimedai siku sio nyingi Cristiano Ronaldo ataiambia dunia kuhusu ujio wa watoto hao.
Kituo cha televisheni cha SIC kimedai hadi sasa hakuna picha hata moja ambayo watoto hao wamepigwa na kikishindwa kufahamu watoto hao wamefichwa wapi kwa wakati huu lakini kikisema wana uhakika na taarifa hiyo ya kuhusu mapacha wa Cristiano Ronaldo.
Hakuna taarifa yoyote kutoka kwa upande wa Ronaldo wala wakala wake kuhusu hilo lakini blogspot kubwa,website na magazeti makubwa ikiwemo gazeti kubwa kabisa nchini Ureno cha Daily Correio Da Manha limeandika kuhusiana na watoto hao.
Ronaldo ambaye kwa sasa ana mpenzi mpya Georgina Rodriguez inasemekana mwanamke ambaye amezaaa naye ni mwenyeji wa bara la America na hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mwanasoka huyu kuzaa na mwanamke asiyejulikana kwani hata mtoto aliyenaye mama yake hajulikani.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t8nINp
via IFTTT


Harmorapa Anusurika Kupondwa Chupa Akiwa Jukwaani..!!!

Harmorapa Anusurika Kupondwa Chupa Akiwa Jukwaani..!!!

Usiku wa Jumamosi hii Harmorapa amenusurika kujeruhiwa vibaya na chupa wakati alipokuwa akitumbuiza katika ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama katika usiku wa Komela.
Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio leo, meneja wa rapper huyo Irene Sabuka amesema, Harmorapa alirushiwa chupa lakini kwa bahati nzuri alikwepa la sivyo yangekuwa yanazungumzwa mengine.
“Kiukweli hili jambo la kusikitisha sana, Harmorapa alikuwa stejini ana perfom ila kabla ya kumaliza show alitokea mtu mmoja akarusha chupa stejini bahati nzuri Harmorapa alikwepa ile chupa. Laiti asingekwepa au ingemkuta kwa bahati mbaya sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine,” amesema meneja huyo.
“Mimi naona kile kitendo ni wivu tu sababu watu hawajui maisha kila mtu ana namna yake anayotokea. Harmorapa ametokea mtaani anatafuta maisha yake leo anaibuka mtu anamrushia chupa na kutaka kumjeruhi, anaibuka mtu mwingine anasema kuwa anataka kumuonesha na kukomesha,” ameongez

from Blogger http://ift.tt/2oDVlFF
via IFTTT


Kategori

Kategori