Showing posts with label 2017 at 02:51PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:51PM. Show all posts
VIDEO:Tundu Lissu Afunguka Mazito Asema ACT Wameanzishwa Kuua Upinzani

VIDEO:Tundu Lissu Afunguka Mazito Asema ACT Wameanzishwa Kuua Upinzani

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki amefunguka kwa kusema chama ACT-Wazalendo kinatumiwa katika kuvunja upinzani uliopo nchini na serikali ya CCM.
Lissu amebainisha madai hayo baada ya Rais Magufuli kumteua aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyeapishwa jana katika viunga vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
“Hao siyo wapinzani hawajawahi kuwa wapinzani, walianzishwa kwa kazi maalumu ya kuua upinzani imeshindikana sasa wanapewa zawadi. ACT na Anna Mghwira walikuwa wakabariane na Lowassa nasiyo CCM walipata kura chache hata laki moja hazikufika. Huu ukuu wa Mkoa ni zawadi tu, Ukatibu Mkuu wa Kitila Mkumbo ni zawadi tu wanawazawadia watu wao hawa siyo wapinzani” alisema Lissu.
Aidha, Lissu amesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi haijawahi kuwa na shida ya aina yeyote na viongozi wa ACT bali shida yao kubwa ni CHADEMA na CUF.
“Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), haijawahi kuwa na shida na ACT wala Kitila Mkumbo, haijawahi kuwa na shida na Anna Mghwira na hao wanaojiita wapinzani wote, shida yao kubwa ni CHADEMA na CUF ndiyo wapinzani wengine wote hawa ni wana CCM” alisisitiza Lissu.
Pamoja na hayo, Lissu amesema haitoweza kuja kutokea kwa Rais Magufuli kuja kumteua yeye kwa nafasi yeyote na endapo itatokea hivyo basi atamtaka kwanza abadilishe katiba mpya ili waweze kutengeza nchi mpya.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s7uU07
via IFTTT


UTAPELI KWENYE MAGROUP YA WHATSAPP

UTAPELI KWENYE MAGROUP YA WHATSAPP

DAR ES SALAAM: Katika kutafuta namna ya kujipatia kipato kwa wakati huu ambapo njia zote za ujanjaujanja zimezibwa na serikali ya awamu ya tano, baadhi ya watu wamebuni mbinu ya kuwatapeli wananchi kupitia makundi ya mitandao ya kijamii hasa WhatsApp.
Kwa mujibu wa mmoja wa watu ambao alijikuta akiingia katika mtego huo kutokana na tamaa yake ya ngono, (jina lake linahifadhiwa) alipata rafiki katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook ambaye baadaye alimweleza kuwa ana mtandao wa wasichana mastaa na wasio mastaa wanaojiuza na angeweza kuwapata kirahisi kwa kupewa mawasiliano yao na pia kuona picha na baadhi ya video wakiwa watupu.
Madai yaliyofikia katika dawati la gazeti hili, vijana wengi ambao ndiyo watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii, wamekuwa wakitapeliwa mara kwa mara kwa kujiunga katika makundi hayo.
Inaelezwa kuwa, mchezo mzima huanzia Mitandao ya Instagram na Facebook ambapo wengi wa matapeli hao huweka picha za wanawake wakali wa Kibongo na kudanganya kuwa wanapatikana kwa njia ya picha na video wakiwa utupu katika makundi yao ya WhatsApp huku wakianika namba za simu watumiwe kiasi cha pesa waunganishwe. Wakishaweka posti hizo katika mitandao hiyo, 
vijana wengi hukimbilia kujiunga kwa kutumia namba zilizowekwa katika mitandao hiyo kwa kiingilio cha kiasi cha kuanzia shilingi 5,000 hadi 10,000 kwa mmoja lakini wakishajiunga katika makundi hayo hakuna kinachoendelea na hata ukiwatafuta hawapokei simu.
OFM KAZINI Katika siku za hivi karibuni ilibainika kuwa, kuna makundi mengi ya WhatsApp yanayoendesha biashara ya ukahaba. Kikosi kazi cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) kikaingia kazini kubaini kama kweli biashara hiyo inaendelea kwa njia ya mtandao ambapo mmoja wa mapaparazi aliomba kuunganishwa na kundi linalojinadi kuwa, ukitaka kahaba wa kila aina unampata.
Kufuatia paparazi kutaka aungwe ili apate huduma,
 alitakiwa kutuma kiingilio cha shilingi 15, akatuma na kuomba aunganishwe na mmoja wa warembo wakali waliokuwa wamewekwa kwenye group hilo. Heh, imeliwa! Baada ya pesa kutumwa, hakukuwa na mawasilino tena na simu ikawa haipatikani.
Ijumaa linawashauri watumiaji wa mitandao hiyo, kuwa makini na watu wa aina hii kwani kila siku wamekuwa wakiongezeka katika mitandao na kujipatia pesa kwa njia rahisi. Ukishaona unaungwa au unashawishiwa kujiunga na kundi ambalo limekaa ‘kihelahela’, akili kumkichwa.

from Blogger http://ift.tt/2nKRmoZ
via IFTTT


Kategori

Kategori