Showing posts with label 2017 at 02:21PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:21PM. Show all posts
TAIFA STARS YAPEWA ZAWADI YA KITITA CHA MAMILIONI YA FEDHA

TAIFA STARS YAPEWA ZAWADI YA KITITA CHA MAMILIONI YA FEDHA

Baraza la Mpira wa Miguu kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa), limetoa zawadi ya dola 10,000 kwa Taifa Stars ya Tanzania baada ya kushinda na kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Castle Cosafa yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.
Fedha hizo ni sawa na Sh. 22,000,000 ambako Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeamua fedha hizo kwa mgawanyo sawa, zitolewe kwa wachezaji wote walioshiriki fainali hizo pamoja na benchi la ufundi.
Kadhalika Cosafa limetuma fedha za zawadi kwa wachezaji wa Tanzania ambao walifanya vema kwenye mchezo mmoja baada ya mwingine katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na mvutio wa aina yake kwa mafanikio ya timu ya Tanzania.
Wachezaji hao ni Shiza Kichuya aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Malawi; Muzamiru Yassin aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola; Erasto Nyoni aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Mauritius; Elius Maguri aliyeibuka Mchezaji Bora wa mechi kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
Kipa Bora wa michuano hiyo ni Said Mohammed alyezawadiwa moja kwa moja na Cosafa. Tanzania ilishika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Zimbabwe na Zambia iliyoshika nafasi ya pili. Tanzania iliifunga Lesotho na kushika nafasi ya tatu.
MABADILIKO MAKUNDI LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA 2017/18
Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko kidogo ya timu zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Timu ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Polisi Morogoro FC ya Morogoro iliyokuwa kundi ‘A’ sasa itakuwa Kundi ‘B’ wakati Mshikamano FC ya Dar es Salaam iliyokuwa Kundi ‘B’ sasa itacheza mechi mechi zake katika Kundi ‘A’.
Kwa msingi huo, makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kund, zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19 yatakuwa hivi:-
Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.
Kundi ‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Polisi Dar za Dar es Salaam na Polisi Morogoro na Mawezi Market ya Morogoro.
Kundi ‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

from Blogger http://ift.tt/2wrMZnv
via IFTTT


YULE MUUGUZI ALIYEMCHOMA MSICHANA SINDANO YA USINGIZI NA KUMBAKA ALALA LUMANDE

YULE MUUGUZI ALIYEMCHOMA MSICHANA SINDANO YA USINGIZI NA KUMBAKA ALALA LUMANDE

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia muuguzi wa kituo cha afya cha Kata ya Igulubi, Damian Mgaya (26) kwa tuhuma za kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 18 baada ya kumchoma sindano ya usingizi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa alisema muuguzi huyo ameshahojiwa na atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika. Alisema msichana huyo amepatiwa fomu ya PF3 baada ya tukio hilo na jana aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya hali yake kuendelea vizuri.
“Hali ya huyu msichana imeimarika na ameruhusiwa, naye atahojiwa kwa upande wake ili tujue uhalisia wa tukio lilivyokuwa,” alisema Kamanda Mutafungwa.
Kamanda huyo alisema siku ya tukio msichana huyo alifika kwenye Zahanati hiyo kumuuguza mama yake mzazi ndipo muuguzi huyo alipotumia nafasi hiyo kumchoma sindano ya usingizi kisha kumbaka.
Ntemi James, ambaye ni Mtendaji wa Kata ya Igulubi amesema tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita kuanzia saa 8 usiku hadi alfajiri wakati msichana huyo akimuuguza mama yake aliyelazwa katika Zahanati hiyo.

from Blogger http://ift.tt/2u9Gyas
via IFTTT


Tetesi za usajili Ulaya zilizovuma hii leo

Tetesi za usajili Ulaya zilizovuma hii leo

Kulikuwa na tetesi za chichini kwamba huenda Anthony Martial akaondoka United na kujiunga na Arsenal lakini leo Mfaransa huyo kutumia ukurasa wake wa Twitter aliandika “Les Remuers Sont Fausses” akimaanisha “tetesi zote ni uongo.”
Pierre Aubemayang inasemekana amepanga kuvitosa vilabu vya Ulaya vinavyomtaka na kusaini nchini China katika klabu ya Tianjin Quanjin ambayo inataka kumsajili Mgabon huyo kwa dau la euro mil 70.
Lakininpia taarifa zinasema mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata ambaye alikuwa visiwa vya Ibiza katika Honeymoon na mkewe ameamua kukatisha Honeymoon hiyo ili kurudi mjini Madrid kujaribu kufanikisha dili lake kuhamia Manchester United.
Wiki iliyopita tetesi zilisema klabu ya Juventus iko tayari kumuuza Alex Sandro kwenda Chelsea kutoka na ofa waliyotuma, lakini sasa dili hilo linaonekana kuwa gumu baada ya Manchester City nao kudaiwa kutuma ofa ya kumnunua Sandro.
Raisi wa Lyon Michel Aulas ameibuka na kudai kwa sasa Arsenal wasahau kuhusu Alexandre Lacazette kwani hakuna dalili ya kuondoka dirisha hili la usajili labda lijalo na akasema dirisha lijalo anaweza kuhamia katika ligi kuu ya Hispania.
Inasemekana klabu ya Manchester United hata ikimsajili Nemanja Matic bado itaendelea kuinasa sahihi ya kiungo wa Monaco Fabinho kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya kiungo
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tpdZpg
via IFTTT


Rapa Chemical Aweweseka Mwenyewe Suala la Rosa Ree

Rapa Chemical Aweweseka Mwenyewe Suala la Rosa Ree

Kwa muda mrefu msanii Chemical amekuwa ndio Rapa pekee wa kike aliyesimama na kuteka wengi, Ila ujio wa rapa mpya Rosa Ree umekuwa mwiba kwake kwani amekuwa akizunguka kwenye media na kumsema kwa jazba kuwa asilinganishwe nae na hata amemuimba kwenye nyimbo 
kimafumbo…Kitu ambacho watu wanadhani kuna bifu kati yao, lakini kwa upande mwingine msanii Rosa ree hajawahi sikika kwenye media akimuongelea chochote..Kwa nanivyo ona Mimi Chemical ni msanii mkubwa si wa kutafuta kiki kwa msanii Mdogo kama Rosa Ree , Rosa ndio alipashwa labda kutafuta kiki kupitia Chemical….Alafu namshauri ni vizuri Ku accept challenges , yeye atoe kazi nzuri mashabiki tutabaki kuwa majaji lakini sio kuweweseka itamtoa nje ya reli..
.
Pendaneni jamani mashabiki tunahitaji marapa wengi wa kike zaidi ya ninyi….
By Bahati

from Blogger http://ift.tt/2oK6O8X
via IFTTT


Mabilioni Yaliyofichwa Kwenye Jumba la Mwanasiasa Yanaswa..!!!

Mabilioni Yaliyofichwa Kwenye Jumba la Mwanasiasa Yanaswa..!!!

Tume ya Uchumi na Makosa ya Kifedha (EFCC) nchini Nigeria, jana usiku ilikamata mabilioni ya fedha za kigeni na fedha za nchi hiyo katika jumba la kifahari la mwanasiasa mmoja.
Maafisa wa tume hiyo walifika kwa kushtukiza katika jumba hilo baada ya kupewa taarifa na ‘Msamalia mwema’ na kunasa zaidi ya $38 milioni, £27,000 na N23 milioni katika jumba hilo lililoko eneo la Ikoyi jijini Lagos.
Waziri wa Habari na Utamaduni wa nchi hiyo, Alhaji Lai Mohammed alisema kuwa mtoa taarifa zilizopelekea kukamatwa kwa mabilioni hayo ya fedha atapewa asilimia tano ya kiasi kilichopatikana.
Serikali ya nchi hiyo hivi karibuni ilieleza faida za watoa taarifa (whistleblowers) na kuahidi kuwa itawalinda.
Serikali ya Nigeria imeeleza kuwa mtoa taarifa zitakazopelekea kupatikana kwa fedha kuanzia Naira bilioni 5, atapata gawio la Naira milioni 210 huku ikiweka wazi jinsi ya kukotoa magawio mengine ya mtoa taarifa kulingana na kiasi cha fedha zitakazokamatwa.
“Kwa mfano, mtoa taarifa akitoa taarifa zitakazopelekea kubainika fedha zilizofichwa kiasi cha Naira bilioni 10, atapata asilimia tano ya Naira bilioni 1 za kwanza, na asilimia nne ya Naira bilioni 4 pamoja na asilimia 2.5 ya Naira bilioni 5 zilizobaki,” Waziri Mohammed anakaririwa na mtandao wa Vanguardngr.
Serikali ya Nigeria inaendesha oparesheni ya kukamata mabilioni yaliyofichwa na watu binafsi majumbani kwa lengo la kuyatakatisha kutokana na biashara haramu na ufisadi, ambapo kabla ya tukio la jana, tume husika ilikamata mabilioni ya fedha za kigeni kwa mmoja kati ya wamiliki maarufu wa maduka ya kubadilishia fedha jijini Lagos.

from Blogger http://ift.tt/2oxot1F
via IFTTT


Kategori

Kategori