Huyu ndio Getruda Nkole wa UVCCM KWAMBE

Katibu wa UVCCM Kata ya Kwembe
Bi. Getruda Nkole Alawa akiwa na mgonjwa Mzee Mnoli 

Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa rehema zake tupo hai na tunaendelea na majukumu yetu vema. 

Katika matembezi yangu ya utafutaji wa Habari za kiutendaji kwa Viongozi wa Chama na Serikali nimejikuta navutiwa na Utendaji wa Katibu wa UVCCM Kata ya Kwembe, Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar Es Salaam. 
Bi. Getruda Nkole Alawa ni Kiongozi shupavu na jasiri sana, Sambamba na mambo mengi afanyayo licha ya nafasi yake ndogo kiItifaki anajitahidi kufanya kazi kwa Weredi mkubwa. 
"CCM oyeeeeee, Nichukue fursa hii kumshukuru Mungu , pia nina  mshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kusimamia haki, pia nimpongeze Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu  Kheri James kwani  ni Kiongozi Mwenye maono na ushawishi mkubwa kwa Vijana wa Tanzania kwa sasa ndani ya muda mfupi wa Uongozi wake.

👉Nakumbuka ilikuwa  siku ya Kongamano la Vyuo na Vyuo Vikuu lililoandaliwa na wana Chuo wa UDSM walipomkaribisha  Mwenyekiti (Kheri James, MCC) ili aje aseme na Vijana. 

Ndipo  nilipokuja  kujifunza zaidi juu ya thamani ya wazazi, Pale Mwenyekiti wa Taifa aliposema..." rudini nyumbani mkapate baraka za Wazazi" 
Kipekee, kabla sijarudi nyumbani nilianza kutembelea majirani zangu kuwajulia hari ndipo  nilipokutana na Mzee aliyeugua muda mrefu bila kupata huduma kwani wanae walimuacha ndani peke yake nikamkuta na shemeji yake Mke wa kaka yake tu akimuuguza tena kwa dawa za kienyej.
" Ndipo  nilipoamua kuchukua hatua  nilienda serikali za mtaa " Kwembe" nikaomba barua ili  akatibiwe bure kwani moja ya sera yetu CCM kwenye Ilani ni Huduma bure kwa Wazee..  nilipata  barua! 
Kabla sijampeleka niliwapigia  simu ndugu zake nikawaambia mimi ni Katibu wa Vijana CCM Kata ya Kwembe,  nikawaambia  kwa mamlaka niliyonayo ninao uwezo wa kuwachukulia hatua kwasababu wamemtelekeza ndugu yao,

 👉 "Wakaogopa" hivyo kesho yake wakanipigia simu na kunijuza kuwa wamempeleka mgonjwa (yule Mzee) "Ruvuma Hospital " iliyopo Kibaha kwa Mfipa, 
Jana amefanyiwa upasuaji, Leo nilienda kumuona na anaendelea vizuri. 

👍Baada ya mgonjwa kufikia  hatua  aliyonayo nimeukumbuka ujumbe wa Mwenyekiti wa Vijana Taifa Ndugi Kheri James wa "Kwenda kwa Wazazi lakini tunapoenda kwa Wazazi tushughulikieni wazazi wa wenzetu ili wazazi wetu watatumiwa watu wengne wa kuwasaidia." 


CCM oyeeeeee najivunia kuwa CCM kwani Leo nilivyofika hospitali kila mtu  Taarifa zangu anazo kwasababu nilishasema mimi ni  Katibu wa UVCCM Kata ya Kwembe. 
Wanaomuuguza mgonjwa wanasema CCM ya sasa hawana masihara ndio maana wamempeleka haraka  mgonjwa hospitali nilipoitaja CCM 😁😁"