WAKULIMA miti ya mbao mkoani Njombe hatarini kuacha kupanda
miti kutokana na miti hiyo wanayo panda kila mwaka kukumbwa na moto kichaa
ambao huiterketeza ikiwana umri tofauti na kuanza upya ama kufa kabisa.
Mwaka jana na mwaka huu moto umetokea katika maeneo mbalimbali
Mkoani Njombe, kwa mujibu wa halmashauri ya wilaya ya Njombe mwaka jana zaidi
ya Hekta 9400 katika katukio tofauti 19 wakati mwaka huu mpaka sasa kuna
matukio 9 ambapo ukubwa tathimini inaendelea kufanyika.
Mwenye mamlaka na misitu halmashauri ya wilaya ya Njombe anasema
kuwa matukio ya moto yamekuwa yakitokea kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo
za kuandaa mashamba ugomvi lakini ili kudhibiti matukio ya aina hiyo tayari
kunahatua ambazo zimeanza kuchukuliwa.
Wataalamu wa misitu na mazingira wanasema kuwa pamoja na
kuteketea kwa misitu na kusababisha hasara za kiuchumi kwa wakulima wa misitu kuna
madhara kwa wanama na wadudu wa porini na kusababisha pia mabadiliko ya hali ya
hewa.
Mkoa wa Njombe ni baarufu kwa ukulima wa miti ya mbao ambayo
huingiza mapato jamii na serikali za halmashauri kwa mkoa huu lakini kwa sasa
sokoni mbao ni nyingi wasiwasi ni ubora
wa mbao hizo kwa kuwa miti inayo vunwa ni kwasababu imeungua na sio kwakuwa
imekomaa.