ZAIDI ya Heka 15,000 za mashamba ya miti mkoani
Njombe ‘sawa na viwanja 150 vya mpira ’ zimeteketea kwa moto katika kata za
Makoga, Kipengele, na Igosi wilayani Wangingombe na kuwasababishia wananchi hao
hasara ya mamilioni ya fedha kutokana na miti hiyo ya kupandwa.
Moto huu Ulizuka juzi majira ya mchana saa sita
mchana na chanzo chake bado kikiwa ni kiulizo kwa wakazi hao kila mkazi akibuni
chanzo chake ikiwa ni pamoja na utayarishaji wa mashamba na wachoma mkaa
wahihisia kuwa ndio chanzo.
Atanasi Mwinuka, ni shuguda wa tukio hilo anasema
kuwa moto huo ulianza kidogo kidogo na baadae kuenea eneo kubwa kutokana na
nyasi kukauka na baadhi ya miti kuwa na asili ya mafuta na kuukuza moto huo.
Alisema kuwa moto huo umekuwa kukisababishw a mara
nyingi na wanao andaa mashamba na kushindwa kuumudu na kuingia katika mapori ya
miti ya kupandwa.
“Wachomba mkaa wamekuwa wakiusahau moto wanao tumia na kusababisha moto kuingia katika nyasi zilizo katika mashamba ya miti na kusababisha majanga kama haya,” alisema Mwinuka.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Njombe ilifika
katika kijiji cha Mwilamba kata ya kipengele kwaajili ya kuuzima moto huolakini
juhudi zikikwama kuumaliza moto huo.
Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka
analiagiza Jeshi la Polisi mkoani Njombe kuhakikisha kuwa chanzo cha moto huo
kinatafutwa ili kudhibiti matukio ya moto.
“Jeshi la Polisi hakikisheni mnafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huu ili kudhibiti matukio kama haya ambayo huwatia hasara wananchi,” Alisema Sendeka
Pamoja na jeshi la polisi kutakiwa kufuatilia
uchunguzi huo viongozi wa kisiasa na watendaji wametakiwa kuhakikisha kutoa
elimu kwa wananchi kuto tumia uandaaji wa mashamba kwa kutumia moto.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Wangingombe, Ally
Kasinge anasema kuwa katika wilaya anasema kuwa matukio hayo yamekuwa yakitokia
mara kwa mara na chanzo kikibwa kikiwa ni wachoma mkaa na waandaaji wa
mashamba.
Kamanda wa jeshi la Zimamoto Mkoani Njombe Deodatus
Ndimbo anatoa tahadhari kwa wakazi wa mkoa wa Njombe kwaajili ya kuepuka
majanga ya moto ambayo huwatia hasara, kwa kuto kumia moto uandaaji wa mashamba.
- Tazama Video stori hii