WAKULIMA wa viazi Mikoa ya Iringa na Njombe
wasanapoteza asilimia 60 ya mapato ya kwenye kilimo hicho kuanzia wakati wa
palizi mpaka mavuno kutokana na uzembe na vitendea kazi duni vya kilimo hicho.
Wakizungumza na startv mkoani Njombe maafisa
kilimo na wataalamu wa viazi wa mikoa ya Njombe na Iringa wamesema kuwa uchafu wa mashamba na vifaa
duni vinavyo tumika katika kilimo cha viazi vimekuwa vikipoteza mazao
Mtaalam wa uzalishaji wa mbegu anasema kuwa mbegu
kitaalamu zimewekewa kiwango cha uzalishaji lakini wakulima wanakosea wakati wa
palizi na kupoteza asilimia 40 na alilimia 10 huachwa shambani wakati wa mavuno.
Sagcot wanatafuta wadau wa kutoa elimu kwa
maafisa kilimo 60 kutoka mikoa ya Njombe na Iringa kwa awamu nne ili kuwasaidia
wakulima kuondoa upotevu huo mafunzo yanayo fadhiliwa na Delphy.
Kilimo cha viazi kwa mikoa ya Njombe na Iringa
kimekuwa kililimwa kwa mazoea na wakulima kutumia mbegu za zamani kitu Kinacho
wasababishia wakulima kuendelea kubaki maskini kutokana na mbegu hizo kutoa
pato duni.