WANAFUNZI 62 wa
shule za sekondari na msingi mkoani Njombe wamebainika wanaujauzito, wakuu wa
shule mkoani humo wametakiwa kuwapima wanafunzi wao kwa kuwashitukiza ili
kuwatio hofu wanafunzi kujiusisha na mahusiani.
Takwimu hizo
zinatolewa na afisa elimu taaluma mkoa wa Njombe, Ambaye amesama kuwa wanafunzi
53 ni wa sekondari na tisa ni wa shule ya Msingi na kutoa maagizo ya kuwapima
wanafunzi kwa kushitukia ili wananzi kuwa na woga wa
kujihusisha na mahusiao huku bwazazi nao wakitakiwa kutoa ushirikiano.
Wakuu wa shule wanasema kuwa kuwapo kwa mabweni
kunaweza kupunguza mimba kwa wanafunzi lakini wazazi nao wanatakiwa kuwalinda
watoto wao na vijana kipindi cha rikizo.
Hayo yanabainika katika mkutano wa wakuu wa shule
mkoa wa Njombe katika mkutano wao chini ya chama chao cha wakuu wa shule
Tanzania Tahosa ambao wanasema kuwa changamoto ni kuwadhibiti wanafunzi ambao
wanatoka nyumbani kuliko wa bweni.
Katika mkutano huu wa wakuu wa shule linaibuka
suala la moto mashuleni ambao kwa mkoa wa njombe ni zaidi ya shule nne
zimekumbwa na majanga ya moto ambako mkoa wa njombe unaagiza kila shule kuwa na
vizimia moto vya mchanga na wakuu kuagizwa kutumia wataalamu katika ujenzi wa
miundombinu ya umeme.