WANANCHI wa mitaa ya Sidon a Buguruni wameishinikiza kamati
ya ujenzi wa zahanati ya Matalawe inayojengwa na mitaa yote miwili kwa madai ya
upotevu wa vitabu vya kukusanyia michango ya ujenzi na kusababisha zahanati
hiyo kuchukuwa mda mrefu kukamilika.
Zahanati hii katika ujenzi wake umeibuka utata wa matumizi ya
fedha za michango ya wadau na kusababisha wananchi kuitaka kamati hiyo kujiuzulu
ili kupisha kamati nyingine.
Pamoja na kuchelewa kwa ujenzi wa Zahanati hiyo wananchi
wanakuwa na wasiwasi wa gharama za ujenzi wa jingo hilo ukilinganisha na
makatilio yao, huku wakihoji ni kwanini maafisa ukaguzi wa ndani wanakuja baada
ya mambo kuharibika.
Baada ya kuwapo kwa utata wa ujenzi wa zahanati hiyo kwenye
matumizi ya fedha mkaguzi wa ndani akapitia matumizi yote na kubaini matatizo
nane katika zahanati yakiwemo ya kutokuwapo kwa kumbukumbu sahihi za fedha.
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo anajiuzulu
nafasi yake ili kupisha wananchi kuchagua kamati nyingine kwa usimanizi na
kusema haya.
Zahanati ya Matalawe ilianza kujengwa mwaka 2010 na
ilikadiliwa kujengwa kwa milioni 60 wakati mpaka sasa imetumia milioni 52 na
bado haijakamilika fedha hizo ni kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali huku
nguvu za wananchi zikiwa hazijaingizwa.