SAKATA LA VYAMA VYA UPINZANI NA JESHI LA POLISI

Jeshi la Polisi limekanusha madai kwamba linalenga na kutumia nguvu kubwa sana kuvinyamazisha vyama vya upinzani nchini na badala yake limesema kuwa linashughulika na watu wanaovunja Sheria na wakikamatwa wanasingizia kuwa ni kwa sababu ya kuwa kwenye upinzani.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi wa Polis (ACP) Barnabas Mwakalukwa alisema hayo jana katika mahojiano na alipokuwa akijitambulisha kwa waandishi wa habari.
Amesema kuwa Jeshi la Polisi halina haja ya kumfatilia mtu yeyote mmoja mmoja lakini huwa linaangalia watu wote ambapo baadhi yao wamo wanaovunja Sheria, amani na kufanya makosa mengine.
Alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa kuhusu ukamataji unaendelea unaohusisha viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani kama Mbunge wa Kawe – Halima Mdee, ambaye alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa saa 48, Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA wakiwa ni baadhi yao.
Alipoulizwa kuhusu tathmini ya Jeshi hilo juu ya hali ya uhalifu nchini, alisema kwamba matukio ya uhalifu nchini yamepungua sana, hasa kwa yale yanayohusu ujambazi wa kutumia silaha na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na wazee.
“Kwa sasa changamoto kubwa ni matukio ya ubakaji kwani yanaongezeka kwa kasi na wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kwa wageni wanaolala majumbani mwao na kwamba wasiwaruhusu kulala kwenye chumba pamoja na watoto wao,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamishna Barnabas, matukio ya ubakaji ya aina hiyo yanayohusisha ndugu yanachukua muda mrefu kuripotiwa polisi na hadi muda yanafikishwa polisi, ushahidi unakuwa ushapotea.
HT @ THE CITIZEN

from Blogger http://ift.tt/2tqVr5d
via IFTTT