POLISI YAWAUWA WAHALIFU WANNE WILAYANI KIBITI

Jeshi la Polisi limewaua watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao walikuwa wakijihusisha na uhalifu katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Pwani.
Watu hao waliouawa katika Kijiji cha Pagae wilayani Kibiti walikutwa na silaha ambayo ni bunduki aina ya SMG na risasi 17 ambazo walikuwa wakizitumia katika matukio mbalimbali ya kihalifu.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mikakati waliyonayo katika kukabiliana na mauaji yanayoendelea mkoani Kibiti.
Miongoni mwa hatua alizosema kuwa wamezichukua ni pamoja na kuanzishwa kwa Kanda Mpya ya Kipolisi Rufiji ambapo Onesmo Lyanga ameteuliwa kuiongoza.
Aidha, Sirro alisema kuwa, endapo wananchi wa maeneo hayo wataamua kuwa kuanzia leo hawataki uhalifu, mambo yote yatakoma kwani kutokana na ushirikiano watakaoupata utasaidia kuwakamata wahalifu wote.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2swUeZ9
via IFTTT