Masauni: Lazima Tushinde vita ya Kibiti

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni amesema kuwa Suala la kumaliza uhalifu kibiti na Mkuranga ni jambo ambalo halina mjadala kwani ni lazima lidhibitiwe.
Mhe. Masauni amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mauaji yanayoendelea maeneo ya Kibiti, Rufiji na Mkuranga.
“Suala la kumaliza uhalifu Kibiti na Mkuranga ni suala ambalo halina mjadala, ni suala la lazima lakini, suala ni lini uharaka wake ndio maana tumejadili changamoto zinazokabili ili tuweze kukaa kwa pamoja tuweze kuzifanyia kazi. Tuweze kuharakisha zoezi hili ambalo kwa hakika kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kwa sisi tunaosimamia haki na uhai wa raia wasio kuwa na hatia hii vita lazima tushinde inshaallah,” alisema Masauni.

from Blogger http://ift.tt/2udjPYT
via IFTTT