KWA NINI WENGINE HUTOKWA JASHO ZAIDI, NA NINI CHA KUFANYA?

Watu wote huwa wanakuwa na idadi karibu sawa za vinyweleo vya kutolea jasho, lakini vifuko vya kutoa jasho huwa vinakomaa miaka miwili ya mwanzo wa maisha. Si vifuko vyote vya jasho vinakuwa na uwezo wa kutengeneza jasho (inategemea mahitaji ya mwili kwa muda huo). Watu wanaoishi kwenye hali ya hewa ya joto huwa wanakuwa na vifuko vinavyofanya kazi zaidi ya waliokua kwenye hali ya hewa ya baridi. Kwa watu wazima, tunakuwa na vifuko vyote lakini ni asilimia ndogo tu ndio vinavyotengeneza jasho.
Hali ya hutokwa jasho zaidi ya wengine (ambayo kitaalamu hujulikana kama hyperhidrosis) ni ya kwawaida ingawa yawezekana ikawa inakusababishia aibu mbele ya wengine. Taarifa kutoka jarida la ‘The Science of Us’ zinaeleza kuwa hakuna sababu za kibaiolojia juu ya hali hii.
Kuna mambo kadhaa yanayousababisha mwili kutoka jasho:
1. Mwili unaanza kutoa jasho hata kabla ya joto kuwa kali sana. Lengo kubwa la mwili kutoa jasho ni kulinda joto la mwili. Kwahiyo, mwili huwa unapokea mabadiliko haraka sana hata kama mabadiliko hayo yakiwa ni madogo katika joto la hali ya hewa. Jasho linaanza kutoka hata kabla hatuaanza kupata kero za joto kali, kwahiyo lile jasho linalokutoka kabla ya hali ya hewa kuwa na joto kali si jambo la kushangaza ila ni jinsi mwili unavyotakiwa kufnaya kazi.
2. Kutokwa jasho kunasababishwa na hali ambazo huwezi kuzitawala, na hali hii imetengenezwa na mwili wako ukiwa mtoto. Hii inamaanisha kuwa kutokwa jasho sana haihusiani na tatizo la kurithi hali hiyo. Kwa hiyo hii inamaanisha kuwa mazingira uliyokuwa ukiishi utotoni mwako ni jambo kubwa sana litalofanya uwe unatokwa jasho kwa kiasi gani katika maisha yako ya baadae.
3. Mwili wako kutoa jasho husaidia vidonda kupona. Vifuko vya jasho vinavyojulikana kwa jina la kitaalamu la “eccrine” ambavyo vinakuwepo kwenye mwili mzima ni muhimu sana kwa kufanya vidonda vikauke haraka. Husaidia sana utengenezwaji wa seli mpya mwilini na kuzitoa zilizokufa kutokana na majeraha ya vidonda. Hii inamaanisha kuwa, vifuko vya jasho ambavyo havitapata nafasi ya kufanya kazi utotoni mwako vitarudisha nyuma uwezo huu mwilini mwako — vifuko vya jasho huwa vinachangia uponyaji wa vidonda mwilini kwa asilimia 100 kwa vijana, lakini uwezo huu hupungua kadri umri unavyoongezeka.
Jinsi ya kupunguza kiasi cha kutokwa jasho jingi mwilini:
1. Unaweza kupunguza kutokwa jasho sana kwa kupunguza muda wa kutumia kiyoyozi. Kama huwa muda mwingi unakuwa kwenye joto la chini (baridi), ni rahisi sana kutokwa jasho pindi joto litakapoongezeka, hata kama ni kwa kiwango kidogo sana.
2. Jiweke kwenye mazingira ya joto kubwa mara kwa mara. Kwa kuongeza kiwango cha joto mara kwa mara (hata kwenye gari yako) mwanzoni itakuletea shida ya kutokwa jasho jingi, lakini baada ya muda mwili wako utazoea hali ya hewa ya joto kali. Kama ukijiweka kwenye joto la juu kwa muda, mwili wako utaizoea hali hiyo.
3. Kunywa maji baridi badala ya kujiwekea barafu kwenye sehemu moja tu ya mwili. Uwezo wa mwili kutoa jasho unategemea joto la ndani ya mwili, sio la nje ya mwili, kwahiyo kunywa maji baridi inasaidia kupoza joto la ndani ya mwili—ambalo kwa kufanya hivyo itasaidia kukuweka sawa bila kujali ugumu wa kazi unayofanay au kiwango cha joto cha hali ya hewa, mwili wako bado utapoa kwa haraka.
Utaratibu huu wa kuufanya mwili kuzoea mabadiliko taratibu pia unatakiwa utumiwe unapoanza kufnaya mazoezi. Kana huwa unatokwa jasho hata unapopanda ngazi chache, hata kama hujachoka, endelea tu kupanda nda ngazi—baada ya muda, yawezekana kwa kupanda ngazi hizo kila siku—mwili wako utazoea na utaweza kupanda ngazi hizo hizo bila kutokwa jasho kwa kiwango ambacho kilikuwa kinatoka mwanzoni mwa zoezi hilo.

from Blogger http://ift.tt/2uA3QHN
via IFTTT