Baba Mzazi akamatwa kwa Tuhuma za Penzi la Mwanaye wa Kumzaa

PWANI: Dunia ime­kwisha! Fadhil Msha­mu, mkazi wa Kibaha Kwa Mfipa mkoani Pwani, Jumanne iliyopita ali­kumbwa na aibu kubwa, baa­da ya kubambwa na polisi, akidaiwa kumshawishi binti yake wa kum­zaa ili ampe penzi.
…Baba huyo akiwa na mwanaye aliyekuwa akimfosi penzi.
UANZE MKASA HUU KWA UMAKINI
K i t e n g o Maalum cha Oparesheni Fi­chua Maovu (OFM) cha Glo­bal Publishers, mwanzoni mwa wiki hii kilipokea simu kutoka kwa mwanam­ke mmoja, ali­yedai wanahitaji msaada kwani katika familia yao, kuna tatizo kubwa ambalo limewasumbua kwa muda mrefu.
… Akiwa katatiwa na polisi.
M w a n ­amke huyo a l i y e d a i a n a i s h i Buguruni jijini Dar es Salaam, alipotakiwa k u d o k e z a tatizo hilo, alidai kuwa ka­tika familia yao, kuna baba anataka kuvunja amri ya sita na binti yake!
OFM WASHTUKA, WATUA BUGURUNI
Kwa taarifa hiyo ya kush­tusha, makamanda wa OFM walilazimika kufika Buguruni ili kupata habari kamili na ku­fika huko, walikutana na mwa­namke aitwaye Tatu Mshamu waliyezungumza naye kwa simu, ambaye alijitambuli­sha kama shangazi wa binti anayetakiwa kutenda dhambi hiyo na baba yake!
HUYU HAPA SHANGAZI
“Huyu ni mtoto wa kaka yangu, kila siku anatuambia baba yake anamsumbua, an­amtaka kimapenzi. Tumejari­bu kukaa naye na kuzungum­za, lakini anatuambia watoto wanamsingizia tu, siyo kweli. Tunajiuliza kwa nini kila siku wakusingizie wewe tu?
“Sasa leo tukaona labda kweli hawa watoto huenda wana lao jambo, tukamwam­bia huyu binti, hebu tuthibi­tishie kama unachoongea ni cha kweli, akasema ngoja apige simu kwa baba yake, akaweka laudi spika!
“Akampigia mbele yetu, tukawa tunamsikia anavyo­mbembeleza. Sasa sisi tu­mechoka, tunataka hili jambo bora lijulikane, maana tume­zungumza naye haelewi, kama mbwai na iwe mbwai tu!”
FAMILIA YAJIPANGA KUMNASA BABA
Wanafamilia hao wali­waambia makamanda wa OFM kuwa walikuwa wame­andaa mtego wa kumkamata baba huyo, kwani tayari al­ishaanza mawasiliano na mwanaye, akimtaka kwenda Kibaha Kongowe ili kwenda kujivinjari naye.
Baada ya kusikia madai hayo mazito na jinsi ya kukutana eneo la tukio, makamanda wetu wakitumia usafiri wao wa mwendokasi, wali­wasili Kibaha Kongowe salama salimini kabla ya kupokea simu kutoka kwa shangazi mtu, aki­waelekeza jina la gesti ambayo baba mzazi alikuwa akimsubiri binti yake.
NEW KILAWENI GUEST HOUSE
Kwa kuwa maka­manda hao walikwi­shamtambua binti huyo anayedai baba yake ku­taka afanye naye ufuska huo, walipofika eneo la tukio, njia ya Soga eneo la Kwa Mmbaga, wal­imuona akiwa amekaa kwenye kiti na meza am­bayo pia aliku­wepo mwa­naume akinywa bia, ambaye kwa harakaha­raka waliamini alikuwa ndiye baba yake mzazi.
POLISI WAIBU­KA, K I Z A A Z A A CHAZUKA
OFM waki­wa hawana hili wala lile, ghafla wakaona kundi la askari zaidi ya nane waki­ibukia eneo hilo, wakiwa w a m e o n ­gozana na shangazi wa binti, Tatu Mshamu na mama mzazi wa binti, An­tonia Mango.
K i t e n d o cha watu hao kuibuka eneo hilo ghafla, kilim­fanya baba mtu kuha­maki, hasa baada ya k u amb iwa kuwa yupo chini ya ulinzi kwa tuhuma ya kufosi penzi kwa binti yake.
ETI WALISHAZAMA GES­TI
Katika hali ya kush­angaza, binti huyo aliua­mbia umati uliokusan­yika hapo kuwa kabla hawajatokea, baba huyo alimpeleka katika chum­ba cha gesti hiyo na ku­taka walale lakini akam­kimbia.
“Alinipeleka chumba namba moja, kulikuwa na kitanda tu, akawa anata­ka tulale, mimi nikakataa, akanifichia viatu vyangu, nikamponyoka nikaja hapa, ndiyo akanifuata akawa ananibembeleza,” alidai binti huyo na ku­waacha watu midomo wazi.
MHUDUMU WA GESTI ASIMULIA
Mhudumu wa gesti hiyo ambaye jina lake ha­likupatikana mara moja, aliwathibitishia polisi kuwa baba huyo alikodi chumba na kuingia na binti huyo chumbani.
AKUTWA NA FUNGUO, ATAITIWA
Huku akiendelea ku­bisha kuwa hakuingia na binti yake chumbani, mzee huyo alikutwa na ufunguo wa chumba namba moja wa gesti hiyo, kitu kilichosababi­sha akose la kusema.
Polisi walimtaiti na kumtaka waelekee chumba walichoingia, ambacho kilikuwa na kitanda tu na kulaz­imishwa kuonyesha alikoweka viatu vya bin­tiye, ambavyo baadaye vilikutwa vikiwa katika kona ya chumba hicho.
SHANGAZI, MAMA
WAZUA TIMBWILI
Kuona hivyo, shangazi na mama mzazi wa binti huyo ambaye kwa sasa alishaachana na mwa­naume huyo, walianza kumshambulia, wakim­tuhumu kuwa anafanya mambo ya aibu.
Timbwili hilo lililoam­batana na maneno maz­ito kutoka kwa mama na shangazi huku baba mtu akijibu mashambulizi, lilichukua muda mrefu kabla ya mtuhumiwa kugeuka ‘mdogo kama piritoni’ kwa aibu.
WASOMBWA POLISI
Kufuatia sakata hilo, maafande hao waliwa­chukua mama, shangazi, binti huyo na baba yake na kuwapeleka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kibaha ambapo baada ya mahojiano walimfun­gulia jadala la uchun­guzi lenye namba KBA/ RB/4067/2017.
Baadaye baba huyo alihamishiwa Kituo Kikuu cha Mkoa na ku­funguliwa jalada ling­ine lenye namba KBA/ IR/2278/2017 JALADA LA UCHUNGUZI.
Mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni haikufahamika kili­choendelea baada ya hapo ila tunaahidi ku­waletea muendelezo wa habari hii kwenye maga­zeti yanayofuata ya Glo­bal Publishers.
chanzo: GPL
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tdYpec
via IFTTT